Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Fainali za mabingwa Afrika kwa vijana chini ya Miaka 17 (AFCON) yanayotarajiwa kufanyika Nchini Tanzania April 2019 yamefikia katika upangaji wa makundi.

Droo hiyo iliyochezeshwa jioni ya leo ikishuhuduwa na viongozi mbalimbali wa Kiserikali wakiongozwa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe na viongozi kutoka Shirikisho la Mpira Wa Miguu Afrika (CAF) pamoja na nchi washiriki waliofanikiwa kuingia katika fainali hiyo.

Fainali hizo zinahusisha timu nane zilizofanikiwa kufuzu na zitachuana kuweza kupata wawakilishi wawili kutoka katika kila kundi kwa ajili ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia la Vijana nchini Peru.Kwenye kupanga makundi hayo mwenyeji Tanzania ameangukia katika kundi la A akiwa na timu za Nigeria, Angola na Uganda.

Katika kundi B, kuna timu za Cameroon , Guinea, Morroco na Senegal.
Waangalizi kutoka CAF wameshakagua viwanja, mahospitali na hoteli kwa ajili ya timu zinazokuja nchini mwakani pamoja na waalikwa kutoka nchi mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...