Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Kikosi cha Yanga kimeendeleza ushindi wake mfululizo na kujikita zaidi kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kushinda mchezo wake dhidi ya AFrican Lyon.

Mchezo huo wa 17 kwa mabingwa hao wa Kihistoria uliochezwa kwenye Uwanja wa Shekhe Amri Abeid Karume Jijini Arusha uliweza kumalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa goli 1-0.

Mechi hiyo ilianza majira ya saa 10 Alasiri, ukiwa ni mchezo wa kasi ya kawaida kila timu ikimsoma mpinzani wake ila kwa Upande wa Yanga waliweza kuwatoa wachezaji wake wawili Jaffar Mohamed na Ramadhan Kabwili baada ya kupata maumivu kwenye Kipindi cha Kwanza.

Mabadiliko hayo Yanga waliyafanya kwa kumuingiza Deus Kaseke na Klaus Kindoki na mpaka mpira unafika mapumziko, kila upande ulikuwa haujaona lango la mwenzake.Kipindi cha Kilianza na African Lyon wakionesha kuhitaji zaidi alama tatu ili kuweka matumaini ya kutoka katika nafasi ya chini huku Yanga nae akitaka kuweka rekodi yake ya kutokufungwa.

Kupitia kwa Beki wake wa Kati Abdalla Shaibu 'Ninja' katika dakika ya 64 aliweza kuiandika Yanga goli la Kuongoza baada ya kuupiga kwa kichwa mpira wa adhabu ulipigwa na Ibrahim Ajib.African Lyon walindelea kusaka goli la kusawazisha na kupata alama moja lakini umakini wa safu ya ulinzi wa Yanga uliwanyima nafasi washambuliaji wake na kupelekea mchezo huo kumalizika kwa kupoteza kwa goli 1-0.

Baada ya ushindi huo, Yanga imefikisha alama 47 wakiwa wamecheza michezo 17 wakishinda 15 na kutoa sare 2, akifuatiwa na Azam mwenye alama 40 akiwa amecheza mechi 16 huki mabingwa watetezi Simba wakicheza mechi 13 na wakisalia nafasi ya tatu kwa alama 30.

Katika mchezo huo uliochezwa Jijini Arusha uliweza kuonesha hamasa kubwa ya mpira wa miguu kwa mashabiki kujitokeza kwa viongozi wa kiserikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo na aliyewahi kuwa Afisa habari wa Yanga na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro.
Kikosi cha Yanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...