SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania-TTCL Corporation linatarajia kufanya matamasha makubwa matatu jijini Dar es Salaam katikaa wilaya za Ilala, Temeke na Kinondoni ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya Rudi Nyumbani Kumenoga, inayofanyika sambamba na kutoa burudani.

Hii ni kuunga mkono hamasa iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli siku ya tar 21 Juni 2018 alipokuwa akipokea gawio la Tsh Bilioni moja na nusu kutoka TTCL Corporation.

Akizungumza leo na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL Corporation, Bw. Ally Mbega alisema tamasha hilo litapambwa na wasanii Shilole, Man Fongo, Belle 9, Dully Skykes pamoja na Chege Chigunda.

Alisema burudani hiyo itaanza siku ya Ijumaa Desemba 21, katika Uwanja wa CCM Mwinjuma, Mwananyamala, na siku ya Jumamosi Desemba 22, Kampenii hizo zitafanyika Wilaya ya Ilala katika Uwanja wa Karume huku fainali za burudani hizo kumalizikia Jumapili Desemba 23, Wilayani Temeke katika Viwanja vya Mbagala Zakhem.

“…Hadi tunavyozungumza leo, Kampeni hii imetembelea Mikoa yote ya Tanzania Bara na Miji mashuhuri na Wikiendi hii ni zamu ya Jiji la Dar Es Salaam. Katika Kampeni za mikoani, tumefanya kazi na Wasanii wawili maarufu, Shilole na Man Fongo.


Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL Corporation, Bw. Ally Mbega akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuzungumzia matamasha matatu makubwa ya kampeni za ‘Rudi Nyumbani Kumenoga’ yatakayoanza Desemba 21, Kinondoni Uwanja wa CCM Mwinjuma- Mwananyamala, Desemba 22 Ilala katika Uwanja wa Karume na Desemba 23 Wilaya ya Temeke viwanja vya Mbagala Zakhem. Kushoto ni Afisa Masoko wa TTCL, Mohamed Shaaban pamoja na Afisa Masoko wa shirika hilo, Bi. Aurelia Boniface (kulia).
Baadhi ya maofisa wa Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL Corporation, wakiwa katika mkutano huo.  


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...