Na Maura Mwingira , Ihumwa Dodoma

Mama Regina (55) ni kati ya akina mama takribani kumi, ambao ni sehemu ya vibarua wanaoshiriki kwa kufanya kazi mbalimbali zikiwamo za kubeba zege katika eneo la Ihumwa inapojengwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Eneo hili la Ihumwa na ambalo lipo takribani kilometa 17 kutoka Dodoma Mjini, limetengwa maalum kuwa Mji wa Kiserikali ambapo kunajengwa Majengo ya Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali. 

“Karibu habari za kazi” ananisalimia mama huyu ambaye anajitabulisha kama Mama Regina wakati nilipomsogelea mahali alipokuwa akichota maji kutoka kwenye simutanki kubwa lililopo eneo la Ujenzi.“ Unataka kunipiga picha” ananiuliza Mama Regina, baada ya kuniona nimeshika Kamera. Ni kamjibu kama yuko tayari na ananiruhusu kumpiga picha”.

Ninapomuuliza kuhusu kazi yake, Mama Regina kwa tabasamu kubwa ananijibu “ Ninamshukuru Mungu, nimefika leo asubuhi na nikabahatika kupata nafasi ya kufanya kazi kwenye ujenzi huu, ninashukuru sana tunafanya hivi kwa ajili ya ada za watoto” anasema Mama Regina kwa furaha kubwa.Furaha ya Mama Regina ya kupata nafasi ya kushiriki kazi ya ujenzi inajithihirisha wazi wazi usoni mwake ni furaha pia inayonekana kwa wamamawegine wanaobeba zege

Anajitishwa ndoo yake ya maji kichwani na kuniambia . “ Mimi nakaa kijiji kingine mbali kidogo na eneo hili la ujenzi, kwa hiyo ilinipasa kufika mapema asubuhi na nikapata nafasi, Kwa kweli nina mshukuru Mungu”
Mwandishi wa habari hii alikuwa miongoni mwa Maafisa wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali waliokwenda jana ( Alhamisi) kuangalia na kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika eneo hilo la Ihumwa.
Akina Mama wakiwa bega kwa bega na  vibarua wenzao wanaume katika  kubeba zege linalotumia kwa ujenzi wa msingi na nguzo  za jengo la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali  katika eneo la Ihumwa nje kidogo ya Jiji la Dodoma
IMG_4604-MACHINE
Kazi ya  uchanganyaji zege ikiendelea katika eneo la ujenzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ihumwa.( Picha na Habari kwa Hisani ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali)
IMG_4647
Mama Regina akijitwika ndoo ya maji na  kuipeleka kunakoojengwa Msingi. Mama Rejina anasema anamshukuru Mungu kwa  kupata fursa ya kushiriki  ujenzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kama ilivyo kwa akina mama wengi, Anasema  kazi hiyo anaifanya kwaajili ya  watoto wake ( ada)
-PICHA 3
Maafisa kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakiangalia na kukagua maendeleo ya ujenzi wa  msingi na usimikaji   wa nguzo mwenye kofia nyekundu ni Injinia  Shadrack Ng’wiza  kutoka Kampuni ya Ujenzi  ya Corporation Sole ( Works Superntent) kutoka Mwanza.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...