Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam
Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) Leo tarehe 21 Disemba 2018 ametembelea studio za Kidigitali za Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na Ukombozi wa Afrika iliyozinduliwa miezi mitano iliyopita na Shirika la Utangazaji Nchini (TBC) katika majengo yake yaliyopo barabara ya Nyerere jijini Dar es salaam.

Mhe Hasunga ametembelea Studio hiyo yenye kuhifadhi historia ya kumbukumbu ya ukombozi barani Afrika zilizopo katika kanda za sauti na video ikiwa imetengenezwa kwa ushirikiano kati ya TBC na Umoja wa Ulaya (EU), Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na wadau wengine wa maendeleo.

Mkurugenzi wa huduma za Redio-TBC Bi Aisha Dachi, amemueleza Waziri wa kilimo kuwa Kuwapo kwa studio hiyo kumelenga kuongeza uwajibikaji, uwezo wa kupata taarifa za zamani na kuongeza uratibu wa menejimenti ya hifadhi ya mambo muhimu ambayo ni ya urithi wa Tanzania.
Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akitazama ubadilishaji wa hotuba za Mwalimu Nyerere kutoka kwenye Analogi kwenda Digitali wakati alipotembelea studio za Kidigitali za Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na Ukombozi wa Afrika zilizopo katika ofisi za Shirika la Utangazaji Nchini (TBC) katika majengo yake yaliyopo barabara ya Nyerere jijini Dar es salaam, Tarehe 21 Disemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Mkurugenzi wa huduma za Redio-TBC Bi Aisha Dachi akimuonyesha Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) mitambo ya makumbusho iliyopo kwenye studio za Kidigitali za Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na Ukombozi wa Afrika zilizopo katika ofisi za Shirika la Utangazaji Nchini (TBC) katika majengo yake yaliyopo barabara ya Nyerere jijini Dar es salaam, Tarehe 21 Disemba 2018.
Mkurugenzi wa huduma za Redio-TBC Bi Aisha Dachi akimuonyesha Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) meza iliyotumiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius  Kambarage Nyerere kwa ajili ya mahojiano iliyopo kwenye studio za Kidigitali za Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na Ukombozi wa Afrika zilizopo katika ofisi za Shirika la Utangazaji Nchini (TBC) katika majengo yake yaliyopo barabara ya Nyerere jijini Dar es salaam, Tarehe 21 Disemba 2018.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...