ALIYEKUWA Naibu Katibu Mkuu wa jumuiya ya Wazazi Zanzibar,Najma Murtaza Giga, amemtaka Naibu Katibu Mkuu mpya wa jumuiya hiyo, Othman Ally, kuendeleza mabadiliko yaliofanyika ndani ya jumuiya ikiwemo kutunza na kuthibiti mali za jumuiya hiyo. Giga alisema jumuiya hiyo kwa sasa inaendana na mabadiliko hayo ambayo jumuiya imeshirikiana na chama katika kuzitunza mali hizo.

Alisema jumuiya hiyo kwa kushirikiana na Chama Cha Mapinduzi(CCM),kimefanikiwa kuwabaini na kuwatia nguvuni waliohusika na upotevu wa mali za jumuiya hiyo hivyo ni vyema kwendana na mabadiliko hayo. Mbali na hilo, Giga alisema jumuiya hiyo iko salama na kwamba hakuna tuhuma zozote zilizoikumba wanachama wa jumuiya katika suala la usaliti na mambo mengine.

Kauli hiyo ameitoa jana wakati akimkabidhi ofisi mjini Unguja ambapo alisema anamkabidhi jumuiya hiyo ikiwa katika hali ya usalama ikiwemo kutokuwepo kwa majungu na makundi. "Hali hii inatokana na kuwepo kwa upendo baina ya viongozi wa jumuiya hiyo ikumbukwe katika jumuiya hii hakuna viongozi waliopatikana na suala la usaliti wa tuhuma zozote zile," alisema.
NAIBU Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar Ndugu Othman Ally Maulid akifafanua namna atakavyoongoza Jumuiya hiyo kwa kufuata Katiba ya CCM ya mwaka 1977 Toleo la mwaka 2017.
 NAIBU Katibu Mkuu Mstaafu wa Wazazi Ndugu Najma Giga akizungumza katika hafla ya mapokezi Naibu Katibu Mkuu mpya ndgugu Othman Ally Maulid katika Kikao cha kujitambulisha kwa viongozi na Watendaji wa ngazi mbali mbali za Jumuiya hiyo hapo Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui.
 VIONGOZI mbalimbali wa Jumuiya ya Wazazi wakisikiliza kwa makini nasaha mbali mbali zinazotolewa na Naibu Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar Ndugu Othman Ally Maulid.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...