Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Februari 8 mwaka huu imepanga kumsomea maelezo ya mashahidi (commital) aliyekuwa Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitillya na mwenzake wawili wanaokabiliwa na mashtaka 58 yakiwemo ya utakatishaji fedha.

Hatua hiyo imefikiwa leo Januari 24,2019 baada ya upande wa utetezi kupinga maombi ya upande wa mashtaka ya kutaka kesi hiyo iahirishwe kwa siku 14 wakieleza kuwa wapo katika hatua za mwisho za kufaili taarifa (fail information), hivyo wanaomba siku hizo kwa ajili ya kukamilisha zoezi hilo. 

Hata hivyo upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili Masumbuko Lamwai ulidai "Washtakiwa hao wamekaa ndani miaka mitatu sasa, walifutiwa kesi kiujanja na kuleta tena kesi hii ili wakae tena ndani, hivi ni kitu gani kinazuia commital, wiki iliyopita walisema leo watawasomea na sasa wanasema wapo kwenye hatua za mwisho watueleze hiyo hatua, " alidai Wakili Lamwai. 

Mapema Wakili wa Takukuru Leonard Swai alidai kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa wanaomba tarehe nyingine ili wakamilishe zoezi la kuwasilisha taarifa kwani wapo katika hatua za mwisho. Hata hivyo, hakimu Huruma Shahidi anayesikiliza kesi hiyo, alikubaliana name upande wa utetezi name kesi hiyo itakuja Kwa ajili ya commital Februari 8, mwaka huu. 

Mbali na Kitilya washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni maofisa wa Benki ya Stanbic, Shose Sinare na Sioi Solomon, Kamishna wa Sera ya uchambuzi wa Madeni kutoka Wizara Fedha na Mipango, Bedason Shallanda na msaidizi wake Alfred Misana.

Katika mashtaka hayo washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matatu ya kughushi, moja la kuongoza uhalifu, 49 utakatishaji fedha, mawili ya kutoa nyaraka za uongo, kujipatia fedha kwa njia ya udanyanyifu moja na shtaka moja la kutoa nyaraka kwa nia ya kumdanganya kwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango. 

Wanadaiwa kati ya Machi 15, 2013 na Januari 10, 2014 ndani ya jiji la Dar es Salaam kwa nia ya kudanyanya washtakiwa wote walijipatia Dola za Kimarekani Milioni sita wakionesha kuwa fedha hizo zilikuwa ni malipo ya ada ya uwezeshaji wa upatikanaji wa mkopo na zililipwa kupitia Kampuni ya Egma T Ltd.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...