Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mh.Simon Odunga amemkabidhi John James zawadi ya baiskeli aliyopewa na Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba Tanzania Ndg.Marco Mtunga ,kwa moyo wake wa kujitolea kwa ajili ya uhamasishaji wa kilimo cha pamba katika kila kijiji wilayani Chemba. 

Mhe.Simon Odunga amekabidhi zawadi hiyo ofisini kwake tarehe 4/1/2019 akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chemba , Katibu Tawala na Wataalam wengine wa Halmashauri ya Chemba. 

Mhe. Odunga amesema” kilimo cha pamba kwa Wilaya ya Chemba wamefanya ndiyo pilot kwa kuanzia Gwandi na ameomba kama inawezekana ndugu James kukopeshwa pikipiki kwa kuwa ndiyo chombo cha pili cha haraka, ni vyema kumkopesha kama mnavyofanya pembejeo kwa wakulima.” 

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Dkt.Semistatus .H Mashimba ameipongeza bodi ya pamba kwa jitihada walizozifanya katika kutoa elimu kwa wakulima hususani kilimo cha pamba na kuwataka vijana wengine wawe mfano hai kama James licha ya kutoa elimu tu bali na kulima kilimo chenyewe . 
Mkuu wa wilaya upande wa kulia Mhe.Simon Odunga akimkabidhi zawadi ya baskeli Ndg .Marco Mtunga aliyopewa kutoka kwa mkurugenzi wa bodi ya pamba tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...