Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) Cliford Ndimbo kuwa Ofisa wa habari wa CAF.
Ndimbo ameteuliwa CAF kuwa OfisA Habari wa CAF katika mchezo wa Klabu Bingwa Afrika utakaopigwa Afrika Kusini.
Ndimbo atakuwa Ofisa kwenye mchezo namba 99 kati ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na Asec Mimosas ya Ivory Coast.
Mchezo huo utachezwa Ijumaa, Februari 1, nchini Afrika Kusini Uwanja wa Tshwane-Loftus Versfeld ni wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Ndimbo anaungana na vigogo wengine kutoka katika Shirikisho la mpira wa miguu Nchini (TFF) kupata nafasi ya kusimamia michezo kadhaa ya Kimataifa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...