Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Waamuzi kutoka nchini Senegal wanatarajiwa kuamua mchezo wa Kundi D wa Ligi ya Mabingwa Afrika baina ya Al Ahly dhidi ya Misri  dhidi Simba ya Tanzani.

Mchezo huo wa tatu wa Kundi D utachezwa Jumamosi ya  wiki hii kwenye Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limewataja waamuzi hao kuwa Utachezwa na mwamuzi Maguette Ndiaye atakayekuwa wa mwamuzi wa kati akisaidiwa na washika vibendera Djibril Camara na El Hadji Malick Samba wakati mezani atakuwepo  Daouda Gueye.  

Simba wamesafiri leo kuelekea Nchini Misri kwenda kujiandaa na mchezo huo wakiwa ugenini na wakisafiri na wachezaji 20 sambamba na benchi la Ufundi na viongozi wengine.

Kwenye mchezo huo Simba wataendelea kuwakosa wachezaji wake nyota Nahodha John Bocco ambaye anauguza majeraha baada ya kuumia kwenye mchezo wao dhidi ya JS Saoura, Erasto Nyoni aliyeumia kwenye kombe la Mapinduzi sambamba na Shomari Kapombe aliyeumia akiwa na timu ya Taifa.

Katika michezo miwili iliyopita Simba walifanikiwa kuondoka na alama 3 wakiwa nyumbani dhidi ya JS Saoura baada ya kuwafunga goli 3-0 na kupoteza mchezo wa pili kwa goli 5-0 dhidi ya As Vita kutoka DR Congo.

Smba anashinda nafasi ya tatu katika Kundi D akiwa alama sawa na As Vita wakitofautiana magoli ya kufunga na Kufungwa na nafasi ya kwanza ikiongozwa na Al Ahly wenye alama nne wakishinda mechi moja na kutoa sare na JS Saoura akishika nafasi ya nne akiwa na alama moja

Mechi hizo zinatarajiwa kuwa zimempa nafasi kocha Patrick Aussems kurekebisha makosa yaliyojitokeza kwenye mechi dhidi ya AS Vita kuelekea mechi ya Jumamosi na Al Ahly.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...