Wakuu
wa Wilaya za Kinondoni, Daniel Chongolo na Wilaya ya Uyui, Gift Msuya
kwa pamoja wamepongeza Juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano katika
kipindi cha mwaka 2018 ambazo zilizolenga kuboresha huduma za jamii na
kuinua maisha ya wananchi.
Akizungumza
leo katika mahojiano maalum na Idara ya Habari-MAELEZO, Mkuu wa Wilaya
ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo, amesema kuwa katika kipindi cha mwaka
2018, wananchi wameshuhudia uboreshaji wa miundombinu ya barabara,
madaraja, vituo vya afya, Elimu, ujenzi Reli ya kisasa, Zahanati na
ujenzi wa Hospitali mpya za Wilaya zipatazo 67.
"Ujenzi
wa reli ya kisasa kwa Kiwango cha Kimataifa (SGR) hapa nchini
utawezesha kufungua sekta mbalimbali ikiwemo uchukuzi, kukuza biashara
kati ya Tanzania na mataifa ya jirani, kufungua uwekezaji ambao
utachochea kwa kiwango kikubwa kukuza uchumi na ustawi wa wananchi",
ameeleza Chongolo.
Akifafanua
kuwa katika Wilaya ya Kinondoni, barabara zenye urefu wa kilomita 58.2
zinaendelea kujengwa kwa kiwango cha lami na baadhi zimeshakamilika.
Ametaja
miradi mingine kuwa ni ujenzi wa Hospitali ya Wilaya inayojengwa katika
eneo la Mabwepande pamoja na ujenzi wa kituo cha afya Kigogo
vitaimarisha na kusogeza karibu huduma za afya kwa wananchi wa maeneo
hayo.Kwa
upande wa maji katika Wilaya ya Kinondoni amebainisha kuwa upatikanaji
wa maji unatarajiwa kufikia zaidi ya asilimia 90 kutokana na maboresho
na uwekezaji ulifanyika katika miundombinu ya maji.
Akizungumzia
Wilaya ya Longido ambayo amewahi kuwa Mkuu wa Wilaya, Chongolo amesema
kuwa kabla ya Serikali ya Awamu ya Tano kuingia madarakani Wilaya hiyo
ilikuwa na Kituo cha Afya kimoja lakini hivi sasa vimejengwa vituo vya
afya vinne vilivyojengwa katika Kata za Kitumbeine, Namanga,
Engarenaibor na Olmoti.
Alibainisha
kuwa upatikanaji wa huduma ya maji Wilayani humo unatarajiwa kufikia
asilimia 130 kutokana na uwekezaji uliofanywa na Serikali katika sekta
ya maji.Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mhe. Gift Isaya Msuya,
ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutoa Shilingi bilioni 1.5 kwa
ajili ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya ambapo tayari maandalizi ya
utekelezaji wa mradi huo mkubwa na wa kihistoria yameanza.
Akizungumzia
mikakati yakuwawezesha wananchi katika Wilaya hiyo, Msuya amesema
tayari Serikali imeendelea kuwajengea mazingira wezeshi wananchi wa Uyui
na mkoa wa Tabora kwa kuimarisha usafiri wa anga ambapo ndege za ATCL
zimekuwa zikifanya safari za mara kwa mara mkoani Tabora jambo
linalochochea maendeleo na ustawi wa wananchi kwa kufungua fursa za
kukuza uchumi.
Ametaja
miradi mikubwa inayoendelea kutekelezwa nchini wa kufua umeme kutoka
Mto Rufiji, Barabara, madaraja, vivuko, na ujenzi na upanuzi wa viwanja
vya ndege katika mikoa mbalimbali hapa nchini kuwa ni mafanikio makubwa
kwa ujenzi wa uchumi na utoaji huduma bora kwa wananchi.
Aidha,
amepongeza hatua ya Mhe. Rais kuwatambua wajasiriamali wadogo maarufu
kama wamachinga kwa kuwapatia vitambulisho maalum
vinavyowawezeshakufanya biashara bila kubugudhiwa hali itakayowainua
kiuchumi na kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato.
Wakuu
hao wa Wilaya wameeleza kuwa kuwa katika mwaka 2019 wanatarajia
kuendelea kutekeleza ahadi za Serikali ili kutoa huduma bora zaidi kwa
wananchi ikiwemo kuweka mazingira bora ya uwezeshaji kuichumi na utoaji
wa huduma za jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...