Nteghenjwa Hosseah, Chemba 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Selemani Jafo amechukizwa na kusuasua kwa ujenzi wa kituo cha Afya Hamai kilichopo katika Wilaya ya Chemba ambacho hakijakamilika ujenzi wa miundombinu ya Afya ilihali fedha za ujenzi zikiwa zimefikishwa kituoni hapo miezi kumi iliyopita.

Mhe. Jafo ameonyesha kuchukizwa kwake wakati wa ziara ya kukagua miradi ya Afya inayoendelea kujengwa katika Halmashauri hiyo mapema leo hii. Akizungumza katika ziara hiyo Mhe. Jafo amesema Kituo cha Hamai kimepokea fedha tangu Januari 2018 lakin mpaka sasa ujenzi haujakamilika wakati vituo vingine vyenye mazingira magumu zaidi vimekwishakamilisha ujenzi tena kwa ubora wa hali ya juu.

Mhe Jafo aliongeza kuwa fedha zilizoletwa hapa ni sh milioni 400 nimeambiwa kuwa zimekwishatumika zote na inahitajika tsh mil 29 zaidi ili kukamilisha majengo haya; Nashindwa kuelewa ni kitu gani cha gharama kilichowekwa katika kituo hiki ambacho kimepelekea fedha hizo kwisha kabla ya ujenzi kukamilika. “Inakuwaje halmashauri zingine wametumia kiasi hicho cha fedha kukamilisha miundombinu yao lakini kwa chemba fedha hizo zisitoshe kukamilisha kituo kuna tatizo gani hapa” alihoji Jafo

Hakuna fedha itakayoongezwa katika kituo hiki cha Hamai nataka majengo yote yaliyojengwa hapa yakamilike haraka iwezekenavyo na kwa ubora unaotakiwa bila kuwa na sababu zingine zozote mkatafute fedha popote mkamilishe kituo hiki aliongeza Jafo. 

 Akizungumza na wananchi wa Hamai Mhe. Jafo aliwajulisha kuwa Halmashauri ya Chemba ni miongoni mwa Halmashauri zilizopata fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya Afya vitatu na Hospital ya Wilaya kwa hiyo hatavumilia kuona fedha hizo zikitumika vibaya atasimamia sharia na atakayekwenda kinyume na maelekezo atachkuliwa hatua kali.
Waziri wa Ncho Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(katikati) akiwasili katika kituo cha Afya Hamai kukagua miundombinu ya afya inayoendelea kujengwa katika kituo hicho kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe. Simon Odunga na kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Mweshimiwa Rajabu. 
Waziri wa Ncho Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akitoa maelekezo baada ya kukagua miundombinu ya afya katika kituo cha Afya Hamai, Chemba 
Waziri wa Ncho Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akitoa maelekezo wakati wa kukagua miundombinu ya afya katika kituo cha Afya Hamai, Chemba 
Mbunge wa Chemba Mhe. Juma Nkamia akizungumza wakati wa ziara ya kukagua miundombinu ya afya iliyofanywa na Waziri wa TAMISEMI Wilayani humo. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...