Na WAMJW - DODOMA
KATIBU Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto-Idara kuu Afya Dkt. Zainab Chaula leo amekutana na Wakurugenzi wa idara na Wakuu wa Vitengo wa wizara hiyo tangu alipoapishwa siku chache kushika nafasi hiyo, akitokea TAMISEMI.
Katika kikao hicho Dkt. Chaula amemshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuendelea kumuamini na kumpa nafasi hiyo, huku akihimiza kila mmoja kufanya kazi kwa ushirikiano na kwa weledi ili kulinda taaluma zao. "Tujiandae kufanya kazi kama timu moja katika kutekeleza sera na miongozo ya sekta ya afya na kuhakikisha dhamana tuliyopewa tunaitumikia kadri inavyowezekana".Alisisitiza Dkt.Chaula
Hata hivyo Dkt.Chaula alimshukuru Katibu Mkuu aliyeondoka Dkt.Mpoki Ulisubisya kwa mifumo mizuri aliyoiweka na kuahidi kuendeleza kwa kuanza na changamoto zilizopo.Aidha,aliwataka wakurugenzi hao kutimiza majukumu yao kwa kufanya kazi kwa kujituma, huku akiwatoa hofu kuwa ofisi yake iko wazi muda wote na yeyote mwenye wazo zuri la kujenga asisite kumuona, kwani lengo ni kuboresha Sekta ya Afya
"uwezo wa kufanya kazi tunao hivyo.mabadiliko ni vitendo, tufanye kazi kwa matokeo". Alisema Dkt. Chaula .Wakati huo huo, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula ametembelea ujenzi wa mji mpya wa Serikali Ihumwa na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Wizara ya Afya.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula (Wakulia) akipokea nyaraka za makabidhiano kutoka kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Ulisubisya Mpoki leo katika Ofisi Kuu za Wizara ya Afya jijini Dodoma.
Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akiteta jambo na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Bakar Kambi baada ya Kikao cha kumkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula.

Kikao chaWakurugenzi, Wakuu wa Vitengo na Wakuu wa Idara Wizara ya Afya kikiongozwa na aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati wakimpokea Katibu Mkuu mpya Dkt. Zainab Chaula leo katika Ofisi Kuu za Wizara ya Afya jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula (Wakulia) akiteta jambo na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Mpoki Ulisubisya leo katika Ofisi Kuu za Wizara ya Afya jijini Dodoma, katika kikao na Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo na Wakuu wa Idara Wizara ya Afya.

Picha ya Pamoja ikiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula, Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya, Naibu Katibu Mkuu Afya TAMISEMI Dkt. Dorothy Gwajima na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Bakar Kambi, pamoja na Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo na Wakuu wa Idara Wizara ya Afya baada ya kikao kifupi cha ukaribisho wa Dkt. Chaula.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula, akiwaonesha namna ya ufuatiliaji ili kuboresha Ujenzi wa Mji mpya wa Serikali Ihumwa wakati alipotembelea ujenzi wa TAMISEMI ili kujifunza, Wakwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Afya TAMISEMI Dkt. Dorothy Gwajima, anaefuata ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Bakar Kambi na Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile akimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula pindi walipokutana kwenye ziara ya kutembelea ujenzi wa Wizara ya Afya katika Mji mpya wa Serikali Ihumwa, jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula (Wakwanza Kushoto) akibadilishana mawazo na aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya (Watatu kulia) pamoja na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Bakar Kambi

Ujenzi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ukiendelea kwa kasi katika Mji mpya wa Serikali Ihumwa, jijini Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...