Badala ya kuendesha shule za kulea watoto kinyemela huko
mitaani, makala haya yatakueleza namna ambavyo unaweza kufanya kusajili na hivyo ukaendesha shughuli hii kihalali.
Ifahamike kuwa ni kosa
la jinai kuendesha kituo au shule ya
kulea watoto bila usajili. Kanuni ya 4(
1 ) ya Kanuni za Vituo vya Kulea Watoto Wadogo Mchana na Watoto Wachanga za
mwaka 2012, zinasema kuwa mtu
hataendesha kituo cha kulea watoto wadogo isipokuwa kama anamiliki cheti halali
cha usajili. Kwahiyo epuka kuingia katika kosa hili kwa kusajili kituo
chako.Makala yatakuwa yakitafsiri Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009, pamoja na
Kanuni za Vituo vya Kulea Watoto Wadogo Mchana na Watoto Wachanga za mwaka
2012.
SIFA ZINAZOHITAJIKA KABLA
YA KUOMBA USAJILI.
1.Eneo ambapo kituo kitajengwa litatakiwa kukaguliwa na
afisa afya wa eneo husika na kutoa ripoti ya kuridhisha kuwa panafaa kwa ajili
ya kulelea watoto. Hii ni kwa mujibu wa kanuni ya 4(3).
2.
Kama eneo/jengo ambapo utaendeshea kituo ni la kupanga basi hakikisha
una mkataba wa pango ambao hauko chini ya miaka mitatu. Kanuni ya 4(4).
3. Utatakiwa kuthibitisha uwezo wa
kifedha kuwa unaweza kuendesha kituo.
4. Hakikisha eneo lina vifaa vya
kutosha kwa ajili ya michezo ya watoto. Hii ni kutoka kifungu cha 47(1)( c ).
5. Muombaji/waombaji wawe na akili
timamu.
6. Uthibitisho kuwa baada ya kupewa
cheti cha kuendesha kituo hautatoa, kuuza, kukodisha kituo au cheti chako kwa mtu mwingine yeyote.
KUSOMA ZAIDI sheriayakub.blogspot.com
Jana tulikuwa na harambee ya uchangishaji wa ujenzi wa kanisa nitakutumia clip hapa
ReplyDelete.