Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Katika kusherehekea miaka mitatu tangu kuanza kutoa huduma zake hapa nchini, kampuni ya mawasiliano ya simu Halotel imefanya tamasha kubwa na la wazi liitwalo “Shukrani Music Concert” katika uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza.

Tamasha hilo limefanyika Januari 12, 2019 ambapo watumiaji wa mtandao wa Halotel walijipatia zawadi mbalimbali ikiwemo simu za mkononi. Aidha kampuni hiyo pia ilitoa mashuka 50 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwanza Sekou Toure na mengine 50 katika Kituo cha Afya Bwisya wilayani Ukerewe.

Makamu Mkurugenzi wa Halotel tawi la Mwanza linalojumuisha mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara, Francis Mafuru alisema kampuni hiyo iliyoanza kutoa huduma zake hapa nchini Oktoba 15, 2015 pia imetumia zaidi ya shilingi Milioni Sita kununua madawa na vifaa tiba kwa ajili ya Kituo cha Afya Bwisya pamoja na Hospitali ya Sekou Toure.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia) ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye tamasha hilo akimkabidhi mwakilishi wa Mgangwa Mfawidhi wa Kituo cha Afya Bwisya, Cosmas Wanzara (kushoto), mashuka yaliyotolewa na kampuni ya Halotel.
Tamasha hilo lilipambwa na burudani kali kutoka kwa msanii Mr. Blue a.k.a BlueByser.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...