Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.
FEBRUARI 15, 2019 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imepanga  kuwasomea hukumu washtakiwa watatu, akiwemo anayedaiwa kuwa malkia wa meno ya Tembo, ambaye ni raia wa China, Yang Feng Glan(66).

Uamuzi huo umefikwa leo Januari 29, 2019 baada ya pande zote mbili, ule wa mashtaka na utetezi kuwasilisha majumuisho yao ya mwisho mahakamani hapo jana (Januari 28, 2019).

Mapema,  Wakili wa Serikali,  Salim Msemo alidai Mahakamani hapo kuwa kesi  hiyo leo ilikuja  kwa ajili ya kutajwa ili iweze kupangiwa terehe kwa ajili ya hukumu.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Huruma Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 15, mwaka huu, itakapokuja kwa ajili ya kuwasomea washtakiwa hao Hukumu. Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Silvanus Matembo Na Philemon Manase.

Katika kesi hiyo, jumla ya mashahidi 11 wa upande wa mashtaka walifika mahakamani hapo kutoa ushahidi wao ambapo washtakiwa walikuwa na hatia na kutakiwa kujitetea ambapo walijitetea wenyewe. 

Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka ya kujihusisha na biashara haramu ya Meno ya Tembo yenye thamani ya Sh 13 bilioni, kinyume cha sheria.

Inadaiwa, kati ya Januari Mosi, 2000 na Mei 22, 2014  washtakiwa walifanya biashara ya vipande 706 vya meno ya Tembo vyenye uzito wa kilogramu 1889, vyenye thamani ya sh. bilioni 5.4 bila ya kuwa na leseni iliyotolewa na Mkurugenzi wa Wanyama Pori.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...