Na Karama Kenyunko globu ya Jamii.
JAJI Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahimu Juma amewataka wasajili wa mahakama zote nchini kuhakiksha kesi zenye dosari haziingii kwenye Mfumo wa mahakama yoyote hapa nchini.
Profess Juma, ameyasema hayo leo Aprili 25.2019 Jijini Dar e Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhudu maadhimisho ya wiki na siku ya sheria nchini, Ambayo hufanyika kila mwanzoni mwa mwaka yanayoashiria kuanza rasmi kwa mwaka wa Mahakama.
Amesema kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu Mahakama ya Rufaa pamoja na mahakama Kuu kutupilia mbali mashauri mbalimbali yanayopelekwa ambapo amebainisha kuwa hali hiyo inatokanana na dosari zinazojitokeza kwe kesi hizo.
Amesema, watu wengi wanalalamikia Mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu kutupilia mbali Mashauri kwa sababu ya dosari zinazojitokeza na kujiuliza kama Mahakama haiko makini ama la.
Muhimbili wa mahakama upo wazi sana, kila kitu tunachokifanya kinapimika, unapofungua kesi unapewa muda wa kujibu, unaleta mashahidi, kesi inarekodiwa, hukumu inatolewa,"Hatupendezwi na malalamiko ya jumla jumla kwani kuna mfumo wa kupokea malalamiko, sisi tupo wazi na
Huwezi kuwazuia Wanasiasa wasizungumze ndio kazi yao, sisi tunafanya kazi kimya kimya na ukitaka majibu utayakuta katika nyaraka" amesema Jaji Profesa Juma.Aidha amemsifu Msajili aliyesimama kidete kukataa kusajili kesi yenye dosari, nampongeza kwa ujasiri, tuna Majaji wachache hatutaki kuwapangia kesi nyingi kisha wazifute" amesema Jaji Mkuu.
Kwa upande mwingine, aJi profesa Juma amewata wananchi ambao wamezoea kubeba mabango ya malalamiko, siku kilele cha wiki ya sheria waache kufanya hivyo na badala yake watumie wiki ya sheria kutafuta suluhu ya malalamiko hayo,ambayo mwaka huu Kitaifa itafanyikia jijini Dodoma katika viwanja vya Nyerere Square kuanzia Januari 31 na kuitimishwa Februari 6.2019 jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika siku ya kilele hicho ambacho kauli mbiu yake itakuwa ni, Utoaji wa Haki kwa wakati: wajibu wa Mahakama na wadau.
Pamoja na mambo mengine Jaji Profesa Juma amesema mashauri mengi ya kesi yanachelewa kumalizika kutokana na uelewa mdogo wa wannchi ikiwa ni pamoja na kutokufahamu miongozo ya mashauri mbalimbali paomja na haki zao.
Achilia mbali hayo pia amebainsha mafanikio ambayo wameweza kuyapata tofuati na miaka mingine ikiwa ni pamoja na kuanzisha matumizi ya usajili wa mashauri kwa njia ya elektroniki huku akisema kuwa licha ya njia hizo bado kasi ya mawakili kisajili mashauri bado ni ndogo
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani).
Msajili wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania, Mhe. John Kahyoza (kushoto) na Mtendaji wa Makhakama Kuu ya Tanzania, Bw. Leonard Magacha (Kulia) wakimsikiliza Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu Maadhimisho ya Wiki na Siku ya Sheria nchini.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi akizungumza wakati wa Mkutano wa Jaji Mkuu na Waandishi wa Habari kuhusu Maadhimisho ya Wiki na Siku ya Sheria nchini.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari wakati wa mkutano kati yao na Jaji Mkuu wa Tanzania.
Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati akizungumza wakati wa Mkutano huo. Kulia ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...