Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii imeishauri Serikali imalize mazungumzo na Benki ya Dunia juu ya hatma ya mkopo wa mradi wa kukuza utalii kwa upande wa kusini baada ya Benki hiyo kuonesha kusuasua kufuatia Serikali ya Tanzania kusimamia uamuzi wake wa kuanzisha Mradi wa kufua umeme wa Mto Rufiji.
Hatua hiyo inakuja baada ya serikali ya Tanzania kukopa jumla shilingi bilioni 345 kutoka Benki ya Dunia ili kukuza utalii katika maeneo ya Kusini kupitia mradi ujulikanao kama Resilient Natural Resource Management for Tourism Growth ( REGROW)
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti Kamati hiyo, Mhe .Nape Nnauye baada ya Kamati hiyo kufanya ziara katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi ikiwa ni moja ya ziara ya kutembelea ukanda wa kusini kwa ajili ya kuona mkopo huo umefikia wapi na namna mradi huo unavyotekelezwa.
Amesema uamuzi huo wa Serikali wa kutaka kufungua Utalii wa Kusini ni wa muhimu sana hata endapo mazungumzo hayo yanayoendelea yatakwama Serikali ifikirie mbadala wake lengo likiwa ni kuongeza mapato yatokanayo na utalii.
Katika mradi huo Hifadhi za Mikumi, Ruaha, Udzungwa pamoja na Pori la Akiba la Selous zinatarajiwa kunufaika kupitia mkopo huo lengo likiwa ni kufanya ukanda wa kusini kuwa lango la Utalii kama ilivyo kwa ukanda wa kaskazini.
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti huyo ameishauri Serikali kuwa endapo fedha za mkopo huo zitapatikana iandae utaratibu wa kuufanya mradi huo uwe wa kibiashara badala ya ilivyo sasa ambapo kwa kiasi kikubwa matumizi ya fedha hizo yamejikita katika uhifadhi zaidi.
Amesema fedha inayowekezwa ni nyingi na italipwa na watanzania sasa ni vizuri itakapowekezwa itoe matokeo yaliyokusudiwa ambayo yatafanana na thamani ya mkopo wenyewe.
Kwa upande wake, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hamis Kigwangalla amesema kumekuwa na mashaka kidogo kutoka kwa Wafadhili ambao wanatukopesha pesa hizo baada ya kuona mradi wa kufua umeme katika mto Rufiji unatekelezwa.
Amefafanua kuwa Wafadhili hao wanahofu kuwa kutakuwa na uharibifu mkubwa wa mazingira na hivyo mradi wa Regrow utashindwa kutekelezwa kwa vile kivutio katika Pori la Akiba la Selous kitabadilika sura yake. Ameelezea kuwa Serikali imefanya jitihada za kuhakikisha kuwa mazingira ndani ya Pori hilo hayataharibiwi na hivyo mradi wa Regrow unaweza ukaendelea kama ilivyopangwa.
Amesema moja ya hatua zilizochukuliwa na serikali ni kuvihamisha viumbe ambavyo vilikuwepo katika eneo linapotarajiwa bwawa kujengwa, Hivyo viumbe hao wataendelea kuwepo na wanaweza kurudi katika eneo lao la awali. Aidha,Mhe.Kigwangalla amesema hata kama itatokea viumbe hao wakapotea kutokana na ujenzi wa bwawa hilo basi viumbe na mimea iliyokuwepo katika eneo hilo vitarudishiwa kwa sababu tayari imechukuliwa na kuhifadhiwa kwenye maabara ya vyuo vikuu mbalimbali vilivyopo hapa nchini kikiwemo Chuo kikuu Cha Dar es Salaam pamoja na Sokoine.
"Tumewaeleza kuwa mashaka yao hayawezi kuzuia huu mradi na bila shaka wametuelewa hivyo tunasubilia uamuzi wa mwisho wa kuamua wanatukopesha au hawatukopeshi" amesema Mhe.Kigwangalla. Pia amesema katika mradi huo yatachimbwa mabwawa makubwa matatu ambayo yatatumika kama vyanzo vya maji kwa wanyama waliopo katika bonde la Mto Rufiji
Akizungumzia manufaa ya mkopo huo , Waziri Kigwangalla amesema utatumika kujenga miundombinu mbalimbali ikiwemo barabara pamoja na viwanja vya ndege ambavyo vitakuwa vichocheo vikubwa katika kukuza na kuendekeza utalii kwa ukanda wa kusini.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii, Nape Nnauye (
wa tatu kushoto) akiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hamis
Kigwangalla pamoja na wajumbe wa kamati hiyo wakipewa maelezo na Mkuu wa
Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, Godwell Meing'ataki kuhusiana na bwawa
lenye viboko wengi katika Hifadhi hiyo liitwalo Mwanambogo wakati
wajumbe ya Kamati hiyo walipofanya ziara ya kutembelea kwa ajili ya
kujionea mradi wa kukuza utalii kusini wa Regrow ulipofikia na namna
unavyotekelezwa.Wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo,
Constantine Kanyasu.( Picha na Lusungu Helela)
Mkuu
wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, Godwell Meing'ataki ( wa kwanza
kushoto)/akitoa Maelezo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu Ardhi,
Maliasili na Utalii, Nape Nnauye, ( wa pili Julia) Waziri wa Maliasili
na Utalii, Dkt.Hamis Kigwangalla ( wa kwanza kulia)pamoja na Naibu
Waziri wa wizara hiyo, Constantine Kanyasu ( wa pili kushoto) kuhusu
uwanja wa ndege unaotarajiwa kuboreshwa na utakuwa na urefu wa kilomita
2.2 unatekekelzwa kupitia Mradi wa kukuza utalii kwa upande wa kusini.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hamis Kigwangalla ( wa nne kushoto) akiwa
kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya
Mikumi jana mara baada ya Kamati ya Bunge ya Kudumu,Ardhi, Maliasili na
Utalii kuondoka katika Hifadhi hiyo.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhe.Nape Nnauye
wakizungumza na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hamis Kigwangalla
pamoja na Mjumbe wa Kamati hiyo Dkt.Steven Kiruswa.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii, Nape Nnauye (
wa tatu kushoto) akiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hamis
Kigwangalla pamoja na wajumbe wa kamati hiyo wakifurahia jambo mara
baada ya kutembelea ziwa la viboko vinavyojulilika Bean a bears kama
maelezo na Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, Godwell Meing'ataki
kuhusiana na bwawa lenye viboko wengi katika Hifadhi hiyo liitwalo
Mwanambogo wakati wajumbe ya Kamati hiyo walipofanya ziara ya kutembelea
kwa ajili ya kujionea mradi wa kukuza utalii kusini wa Regrow
ulipofikia na namna unavyotekelezwa.Wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa
Wizara hiyo, Constantine Kanyasu.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhe.Nape
Nnauye ( wa pili kushoto) Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hamisi
Kigwangalla ( wa tatu kushoto) wakiwa pamoja na viongozi wengine
wakizungumza mara baada ya kkuhitimisha ziara katika Hifadhi ya Taifa ya
Mikumi mkoani Morogoro.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...