Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
WATU wamefurika katika nyumba ya kuhifadhia maiti Chimoro Nairobi kutambua miili ya ndugu zao  waliouwawa katika shambulio la kigaidi lililotekelezwa na kundi la Al shabab.

Rais Uhuru Kenyatta  amehutubia taifa na kueleza kuwa watu 14 wamefariki katika shambulio hilo huku watu zaidi ya watu 700 wakiokolewa.
Kenyatta ameeleza kuwa operesheni hiyo imekamilika na waliotekeleza shambulio hilo wameuwawa na amewahakikishia usalama wakenya wote huku wanasiasa wakizuiliwa kuingia mahali hapo.

Aidha umoja wa Afrika (AU) na Marekani kupitia balozi wao nchini humo Robert Gidec wamelaani vikali tukio hilo la kigaidi lililogharimu maisha ya wengi.

Pia imeelezwa kuwa kamera za usalama (CCTV) zimenasa video ambayo inaonesha magaidi wanne wakiingia katika viunga vya hoteli hiyo na maafisa wa polisi wamegundua nyumba iliyokuwa mita chache kutoka eneo la tukio ambayo inasadikika kutumika kwa kupanga mbinu hizo za uvamizi.

Chanzo: The StandardMedia

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...