KARATU: RIPOTI ya utafiti mdogo unaolenga kujua miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA), kwa Tarafa ya Ngorongoro huenda ikatoa mwelekeo wa kutatua changamoto za miaka mingi kwenye eneo hilo. Matokeo ya awali ya utafiti huo yalitolewa mjini Karatu na jopo la Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) waliopewa jukumu na NCAA iliyohitaji kuona endapo kuna mafanikio na mapungufu kwa kiwango gani.

Kwa miaka mingi NCAA imekuwa ikitenga mabilioni ya fedha kwa ajili ya bajeti ya maendeleo ya jamii na uendeshaji wa shughuli za Baraza la Wafugaji (NPC), linaloundwa na wafugaji wanaoishi Tarafa ya Ngorongoro. Jopo la watafiti hao liliongozwa na Mtaalamu wa Mifugo na afya za wanyama Professa Saradhili Kimera, Mtaalamu wa Nyanda za malisho Dk. Anthony Sangeda, Dk. David Mushin a Dk. Said Mmbaga wote kutoka SUA.


Akiwasilisha ripoti hiyo Prof. Kimera alisema, NCAA iliomba ushauri SUA wa kutengenezwa utafiti mdogo wa kujua miradi wanayoifanya ya kusaidia jamii hasa katika mifugo imeweka maboresho ya aina gani, mapungufu na mafanikio yepi. Kwa upande wake Naibu Kamishana wa Uhifadhi NCAA Dk. Maurus Msuha alisema ripoti hiyo imegusia masuala muhimu ikiwamo ushauri wa kupunguza mifugo kwa wakazi.

“Ukiangalia idadi ya ongezeko la mifugo, watu, ongezeko la mahitaji ya jumla na mabadiliko ya tabia nchi.

“Lakini pia unapokuwa na mahitaji ya uhifadhi na utalii una imarika kwa kupata mapato ya kuendeleza watu walio ndani ya hifadhi lazima uwe na mipango madhubuti ya kuhakikisha mambo yanakwenda sawia.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Wafugaji Tarafa ya Ngorongoro Edward Maura aliwapongeza wataalamu hao kwa kuja na ripoti iliyochambua kwa uwazi uhalisia na uwazi wa maisha ya Ngorongoro. 
Viongozi wa Baraza la Wafugaji Tarafa ya Ngorongoro, Watendaji wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA), Viongozi wa Chama cha Mapinduzi wilaya na Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine Morogoro (SUA) wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa wasilisho la awali la ripoti ya utafiti kuhusu eneo la Hifadhi.
Professa Saradhili Kimera kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) akiwasilisha ripoti ya utafiti unaolenga kujua miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) katika Tarafa ya Ngorongoro chini ya ushirikiano wa Baraza la Wafugaji wa Tarafa hiyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro akizungumza wakati wa wasilisho la utafiti uliofanywa na wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) unaolenga kujua miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) katika Tarafa ya Ngorongoro chini ya ushirikiano wa Baraza la Wafugaji wa Tarafa hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...