*Asema uhusiano kati ya CAG na Bunge ni muhimu, akiri hakuwa na nia ya kulidhalilisha Bunge

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad amekubali mwito wa Spika wa Bunge 

Job Ndugai la kumtaka kufika kwenye Kamati ya Haki,Kinga na Madaraka ya Bunge Januari 21, 2019 ili ahojiwe na kamati hiyo.

Spika Ndugai alitangaza kumuita Profesa Assad kwenye kamati hiyo baada ya kudai kuwa amelidhalilsha Bunge kutokana na kauli yake ambayo ameitoa nchini Marekani ya kwamba Bunge ni dhaifu.

Akizungumza leo Januari 17, 2019 Profesa Assad amesema Ofisi ya CAG na Bunge ni taasisi ambazo lazima zimefanye kazi zake kwa karibu sana na kwamba anaamini kuwa mpaka sasa ana mahusiano mazuri na yenye tija na si tu kwake na Spika bali ni Bunge zima la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

"Pia mimi na wakaguzi wangu tumekuwa tukifanya kazi vizuri pamoja na kuaminiana kati yetu na wenyeviti na wajumbe wa Kamati zote za Bunge "amesema Profesa Assad na kuongeza kuwa uhusiano kati CAG na Bunge ni 
wenye umuhimu katika kutekeleza majukumu yake kikatiba na mantiki hiyo ni lazima uenziwe na kudumishwa na yanayotokea hivi sasa hayafurahishi bali yanasikitisha.

Aidha Profesa Assad amesema katika mahojiano yake yaliyozua mjadala hayakuwa na nia ya kudhalilisha Bunge hata kidogo na kufafanua maneno kama udhaifu na mapungufu ni lugha ya kawaida kwa wakaguzi katika kutoa maoni ya utendaji wa mifumo ya taasisi mbalimbali.

Hata hivyo amesema kuwa ni wazi kwamba watu wengine wanaweza 
kuchukua tafsiri tofauti ya maneno kama hayo. "Hivyo naitikia mwito wa Janauari 21".
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad  akizungumza na waandishi wa habari (hawapo picha)leo jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,(MMG)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...