Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Watoto kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bwa. Sebastian Kitiku amesema karibu nusu ya wanawake mkoani Dodoma wameolewa wakiwa chini ya umri wa miaka 18.

Akifafanua kuhusu hali ya mimba na ndoa za utotoni katika Mkoa wa Dodoma Bw. Kitiku alisema kati ya wanawake 100 waliolewa mkoani Dodoma 51 kati yao waliolewa na umri chini ya miaka 18 na kati ya wazazi 100 mkoani Dodoma wazazi 45 kati yao wamepata mimba za utotoni.

Mkurugenzi huyo alisema hayo mjini Dodoma wakati wa kikao kazi cha kuandaa ujumbe wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto kama hatua ya umuhimu ya kutekeleza Mkakati wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto mkakati unaotekelezwa kwa kipiandi cha miaka mitano.

Aliutaja mkoa huo pia kuwa unakiwango cha juu cha ukeketaji jambo linafanya mkoa huo kuwa katika nafasi za juu katika viwango vya ukatili Nchini kwani takwimu zinaonesha Mkoa uko katika nafasi ya 2 kitaifa kwa kuwa na asilimia 41 ya vitendo vya ukeketaji akitaja Manyara kuwa na kiwango cha juu zaidi kwa ukeketaji ikiongoza kwa asilimia 58.

‘’Sisi wataalamu tunachukulia ukeketaji kama ukatili dhidi ya watoto kwani unakiuka haki ya msingi ya ulinzi watoto kwa kuwa ukatili una madhara kiafya na kisaikolojia kwa binadamu akiwa mtoto na akiwa mtu mzima pia kwani anabaki na makovu moyoni kipindi chote cha maisha yake.”Alisistiza Bw. Kitiku.

Ameitaja Dodoma kuwa iko katika mikoa inayoongoza kitaifa katika suala la ndoa za utotoni ikiongozwa na Katavi  ambayo takwimu zake kwa ndoa za utotoni ni asilimia 45 lakini pia mkoa wa Dodoma una kiwango cha juu cha ukeketaji na mimba za utotoni.

Kazi ya kutengeneza ujumbe kwa ajili ya kutokomeza mimba na ndoa za utotoni pamoja na ukeketaji  inaendelea tayari imefanyika  katika mikoa yenye takwimu za juu katika ukatili dhidi ya wanawake na watoto ambayo ni mikoa ya Shinyanga, Tabora, Singida na Rukwa na sasa Dodoma na jumbe hizi zikikamilika zitatumika katika kuhakikisha vitendo vya ukatili vinapungua kwa kiwango kikubwa au kwisha kabisa.  
 Mkurugenzi Msaidizi Idara ya watoto kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Sebastian Kitiku akiongea wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha watendaji wa Mkoa wa Dodoma pamoja na Wizara ya Afya kujadili jumbe za kuelimisha jumii kuhusu ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
 Baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha watendaji wa Mkoa pamoja na Wizara ya Afya wanaokaa katika Jiji la Dodoma kujadili jumbe za kuelimisha jumii kuhusu ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha watendaji wa Mkoa pamoja na Wizara ya Afya wanaokaa katika Jiji la Dodoma kujadili jumbe za kuelimisha jumii kuhusu ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...