Na Amisa Mussa

Naibu Waziri Wa Mifugo Na Uvuvi Adballah Ulega amesema kuna haja ya kufanya mazungumzo ya kina na Wizaraya Ujenzi na Mawasiliano kuhusu Kuishauri Wizara hiyo kuona umuhimu wa kufufua Miundombinu ya kupakia na kushusha Ng'ombe Wanaosafirishwa Kupitia Usafiri Wa Treni Ya Mizigo Hatua Ambayo Itasaidia Kupunguza Adha Kubwa Ya Usafishaji Mifugo Wanayokumbananayo Wafanyabiashara Ya Ng’ombe.

Naibu Waziri Ulega ameyasema hayo wakati alipotembelea kituo  cha usafishaji cha Reli ya Kati Mjini Tabora na Kukagua Miundombinu ya Kupakia Na Kushusha Ng'ombe Wanaosafirishwa Kwa Usafiri Wa Treni.

Aidha Miundombinu Katika Kituo Cha Usafirishaji Cha Reli Ya Kati Mjini Tabora Inaonekana Kusahaulika Ambapo Naibu Waziri Huyo Amesewasihi Wafanyabiashara Ya Ng’ombe Wilayani Humo Kuendelea Kufanya Biashara Katika Mnada Wa Ipuli.

Awali Mkuu Wa Wilaya Ya Tabora Mjini KOMANYA ELIC KITWALA Na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Tabora LEOPAD ULAYA Wamesema Miundombinu Inayotumiwa Na Wafanyabiashara Na Wafugaji Wa Ngombe Ni Finyu Hatua Ambayo Inasababisha Wafanyabiashara Hao Kupata Usumbufu Wawapo Kituoni Hapo

Aidh Naibu Waziri Ulega amewasihi Wafanyabiashara wanaotumia Mnada wa Ipuli Mjini Tabora kufuata  na kuzingatia Sheri, Kanuni na Taratibu ili kuepuka Migongano isiyokua ya lazima.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...