Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania ( TTCL), Mhandisi Omary Nundu (kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka jipya la TTCL lililopo Kariakoo Mtaa wa Mafia na Msimbazi leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba akishuhudia tukio hilo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania ( TTCL), Mhandisi Omary Nundu (kushoto) akizungumza katika uzinduzi wa duka jipya la TTCL lililopo Kariakoo Mtaa wa Mafia na Msimbazi leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Bw. Waziri Kindamba pamoja na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa TTCL, Ndugu Ally Mbega (kulia).
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania ( TTCL), Mhandisi Omary Nundu (kulia) akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa TTCL wanaotoa huduma ndani ya duka hilo jipya la TTCL lililo zinduliwa leo eneo la Kariakoo Mtaa wa Mafia na Msimbazi jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania ( TTCL), Bw. Waziri Kindamba (kushoto) akizungumza katika uzinduzi wa duka jipya la TTCL lililopo Kariakoo Mtaa wa Mafia na Msimbazi leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la TTCL, Mhandisi Omary Nundu akimsikiliza.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania ( TTCL), Mhandisi Omary Nundu (kulia) akiingia kwenye duka hilo mara baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania ( TTCL), Mhandisi Omary Nundu (wa pili kulia) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Bw. Waziri Kindamba (wa pili kushoto) wakionesha baadhi ya bidhaa za TTCL zinazopatikana katika duka jipya la TTCL lililozinduliwa leo eneo la Kariakoo Mtaa wa Mafia na Msimbazi jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa TTCL, Ndugu Ally Mbega (kulia) pamoja na Kaimu Mkuu wa Biashara Kanda ya Dar Es Salaam, Bi. Jane Mwakalebela.
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Bw. Waziri Kindamba, Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania ( TTCL), Mhandisi Omary Nundu pamoja na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa TTCL, Ndugu Ally Mbega wakionesha baadhi ya bidhaa za TTCL zinazopatikana katika duka jipya la TTCL lililozinduliwa leo eneo la Kariakoo Mtaa wa Mafia na Msimbazi jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa duka jipya la TTCL lililo zinduliwa leo eneo la Kariakoo Mtaa wa Mafia na Msimbazi jijini Dar es Salaam.



SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) leo limezinduwa duka jipya na kituo cha huduma Kariakoo eneo la Mtaa wa Mafia na Msimbazi jijini Dar es Salaam ikiwa ni jitihada za kusogeza huduma zake karibu zaidi na wateja.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania ( TTCL), Mhandisi Omary Nundu alisema kwa Mwaka 2019, TTCL imejipanga vyema kuhakikisha kuwa Huduma za Shirika hilo zinasambaa zaidi kote nchini huku ikisimamia ubora na unafuu wa gharama ambazo zitakuwa nafuu kwa wananchi.

"...Tunakusudia kuendelea kufanya mageuzi makubwa ndani ya Shirika ili kuliwezesha kushindana kikamilifu katika Soko la Huduma za Mawasiliano Nchini sambamba na kutimiza wajibu wa kimsingi wa kuwa mchangiaji muhimu katika Pato la Taifa," alisema Mhandisi Omary Nundu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Corporation, Bw. Waziri Waziri Kindamba awali akizungumza alisema uzinduzi huo wa duka na kituo cha Huduma kwa Wateja ni utekelezaji wa Mpango Mkakati wa miaka mitatu, 2016-2019 ambao umeweka msisitizo mkubwa katika kuboresha eneo la Huduma kwa Wateja.

"Uzinduzi wa leo unaonesha kwa vitendo jinsi gani TTCL mpya ilivyojipanga vyema kuhakikisha huduma zake zinawafikia Wateja katika mazingira mazuri, yanayovutia na kuwakilisha hadhi ya Shirika letu. Kukamilika kwa Duka hili/ Kituo hiki cha Huduma kwa Wateja kuonaongeza idadi ya Maduka mapya ya TTCL kufikia maduka 10 ambayo yamejengwa kwa viwango vya hali ya juu na kwa kuzingatia mahitaji ya sasa ya utoaji bora wa Huduma kwa Wateja,"

Aidha aliongeza kuwa TTCL itaendelea kuboresha Maduka na Vituo vyetu Nchi nzima, sambamba na Ofisi zake za Mikoani na Wilayani ili ziweze kuwa mahali bora kabisa kwa Watumishi wa TTCL wanaotoa huduma na Wateja wote watakaofika kupata huduma za aina mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...