Na Karama Kenyunko Globu  ya Jamii.
MAHAKAMA  ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA), Dickson Maimu na wenzake 6 waliokuwa wakikabiliwa na kesi  ya uhujumu uchumi na kusababisha hasara ya Sh.Bilioni 1.16 kwa sababu Mkurugenzi wa Mashtaka' (DPP) hana nia ya kuendelea  na mashtaka dhidi ya washtakiwa

Washtakiwa hao wameachiwa chini ya kifungu cha 91(1) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sura 20 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002. Hata hivyo,  mara baada ya vigogo hao kuachiwa  huru na kutoka nje ya chumba cha mahakama, walikamatwa tena na kuwekwa chini ya ulinzi na polisi na baadae kupelekwa katika kituo cha polisi cha Kati

Mapema wakili wa serikali Wankyo Simon akisaidiana na Leornad Swai kutoka Takukuru aliileza mbele ya Hakimu  Mkazi Janet Mtega kuwa kesi hiyo leo imekuja kwa kutajwa, "Mheshimiwa shauri hili linakuja kwa kutajwa lakini DPP hana nia ya kuendelea shtaka dhidi ya washtakiwa, tunaliondoa chini ya kifungu cha 91(1) cha mwenendo wa makosa ya jinai kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

 Hakimu Mtega alikubali ombi hilo na kuliondoa shtaka hilo
Hata hivyo, washtakiwa baada ya kuachiwa wamekamatwa tena na kupelekwa kituo cha polisi cha kati. Kesi hiyo ilifikishwa kwa mara ya kwanza  mahakamani Agosti18, 2017 lakini hadi leo upelelezi bado haujakamilika.

Washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo mbali na Maimu ni Meneja Biashara wa (NIDA), Avelin Momburi na Mkurugenzi wa TEHEMA, Joseph Makani
Awali washtakiwa hao walikuwa nane lakini sasa wamebaki saba kwa sababu mmoja ambaye alikuwa Kaimu Mhasibu Mkuu wa NIDA, Benjamin Mwakatumbula alifariki dunia.

Wengine ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers,  Astery Ndege, Ofisa Usafirishaji, George Ntalima, Mkurugenzi wa Sheria, Sabina Raymond na Xavery Kayombo.

Katika kesi hiyo, washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka ya kutumia madaraka vibaya, kula njama, kutumia nyaraka za uongo kumdanganya mwajiri na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh 1,169,352,931.

Inadaiwa kwenye shtaka la kwanza Maimu na Mwakatumbula kati ya Januari 15 hadi 19,  mwaka 2010 katika makao makuu ya NIDA  wilayani Kinondoni Mkoa wa Dar es Salaam, wakiwa watumishi wa umma kwa nafasi walizokuwa nazo  walitumia madaraka  vibaya.

Wanadaiwa kuwa waliidhinisha malipo kwa Gotham International Limited (GIL) ya Dola za Marekani 2,700,00 bila ya kutumia viwango vya kubadilisha fedha za kigeni vilivyowekwa na  Benki Kuu ya Tanzania,    kinyume na kifungu 19.3 cha mkataba kati ya NIDA na GIL, hivyo kuifanya GIL kupata faida ya Sh 3,969,000.

Maimu na Mwakatumbula katika shtaka jingine wanadaiwa kati ya Juni 3 na 5, 2013 katika makao makuu hayo walitumia madaraka vibaya kwa kuidhinisha malipo kwa GIL ya Dola za Marekani milioni 1.8, bila ya kuzingatia viwango vya kubadilisha fedha, hivyo kuifanya GIL kupata faida ya Sh 106,346,000.

Washtakiwa hao wawili wanadaiwa Juni 20, 2014 katika makao makuu hayo, waliidhinisha tena malipo ya Dola za Marekani 675,000 kwa GIL bila ya kuzingatia viwango vya kubadilisha fedha, hivyo kuifanya kampuni hiyo kupata faida ya Sh 42,471,000.

Maimu na Mwakatumbula wanadaiwa kutumia madaraka yao vibaya kwa kupitisha malipo mengine ya Sh6 milioni  kwa GIL bila ya kupiga  hesabu kwa kutumia viwango vya kubadilishia fedha hivyo kuifanya kampuni hiyo kupata faida ya Sh 14, 661,676.76.

Maimu na Mwakatumbula wanadaiwa kati ya Januari 15, 2010 na Mei 16, 2015 katika makao makuu hayo ya NIDA kwa kuidhinisha malipo kwa GIL ya Dola za Marekani bila ya kuzingatia viwango vya kubadilisha fedha za kigeni waliisababishia NIDA kupata hasara ya Sh 167,445,676.76.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...