Selina
Mushi wa Mlandizi Njia Panda JKT anasikitika kutangaza kifo cha mume wake
mpendwa Clement Thomas Ndeleokasi Shayo kilichotokea Alhamsi tarehe 29, Novemba 2018
katika hospitali ya Muhimbili - Mloganzila.
Mazishi yalifanyika nyumbani kwa
marehemu, Uparo-Kirua Vunjo Moshi, Kilimanjaro siku ya Jumanne tarehe 4 Desemba,
2018. Watoto wa marehemu, Frederick Clement Shayo na Regina Clement Shayo,
pamoja na mama yao Selina Mushi na dada wa marehemu Clementina Thomas
Shayo wakishirkiana na famlia ya Mtika
na ukoo wote wa Shayo, pamoja na familia ya Lesiaki Mushi wanatoa shukrani za dhati
kwa wauguzi wa hospitali ya Muhimbili-Mloganzila kwa juhudi zao za kujaribu
kuokoa maisha ya mpendwa wao Clement.
Shukrani zao za pekee zinatolewa kwa
Sista Agatha wa kituo cha Afya cha Mtakatifu Joseph, Luguruni Dar es Salaam, ndugu,
jamaa na marafiki wote waliomhudumia Clement wakati wa kuugua kwake. Marehemu aliugua akalazwa hospitali kwa muda
mfupi na kuruhusiwa; kisha akapata stroke.
Kifo cha Clement kimekuwa mshtuko mkubwa kwa
ndugu, jamaa, marafiki, na wote waliomfahamu Tanzania, Marekani na Canada.
Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa, Jina Lake Lihimidiwe. Mwenyezi Mungu aipokee roho
ya marehemu Clement katika Furaha ya Milele, Amina
Rest In Peace Mr Shayo! Poleni sana familia yake na ndugu na jamaa wote.
ReplyDelete