Na Wankyo Gati,Arusha 

JAJI wa Mahakama ya Rufani Tanzania,Dk.Gerald Ndika amesema kuwa, serikali inatekeleza mikataba ya kimataifa hususani ile ya kuondoa unyanyasaji wa wanawake kwa kukusanya taarifa za unyanyasaji na kuzifanyia kazi ili kutokomeza vitendo vya unyanyasaji na ukatili dhidi ya wanawake.

Akizungumza katika Mkutano wa kimataifa ulioangazia masuala ya Utoaji haki kwa wanawake kupitia mifumo ya kimahakama uliondaliwa na Shirika la kimataifa linalojihusisha na masuala ya Wanawake pamoja na Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania ,Dk.Ndika alisema kuwa, tayari serikali imeridhia mkataba huo ambao unatekelezwa kwa dhana shirikishi ambapo Mahakama,Wizara ya Katiba na Sheria,Wizara ya Afya na Asasi za kiraia ambazo hutumika kukusanya taarifa ambazo nchi inaziwasilisha .

Dk.Gerald alisema kuwa ,juhudi endelevu zinahitajika katika kupiga vita vitendo vya unyanyasaji wa wanawake pamoja na kutathmini utekelezaji wa mikataba hiyo ili iweze kuzaa matunda.

Kwa upande wa Jaji Kutoka Mahakama Kuu Tanzania Joaquine De Mello amesema kuwa, changamoto za mila na desrturi imekuwa kikwazo katika kutetea haki za wanawake jambo ambalo linahitaji ushiriki mpana.

Alisema kuwa, sheria ya ndoa na sheria ya mirathi inapaswa kuangaliwa upya kwani kuna baadhi ya vipengele vina mkandamiza mwanamke na kumnyima haki zake za msingi. 

Afisa Programu wa Shirika la kimataifa linalojihusisha na mambo ya Wanawake (UN WOMEN) ,Rachel Boma alisema kuwa, Tanzania imeridhia sheria mbalimbali za kimataifa kwenye eneo la kutoa haki kwa wanawake lakini bado kuna baadhi ya sheria ambazo ni kandamizi ikiwemo sheria ya mirathi na sheria ya ndoa .

Aidha alisema kuwa, katika kutafuta ufumbuzi wa kudumu hivi sasa wizara ya sheria ipo katika mikakati wa kufanya marekebisho katika sheria ya mirathi na ndoa ili kuweza kuondoa baadhi ya vipengele kandamizi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...