Na Woinde Shizza Globu ya jamii ,Arusha.
Wanawake wajasiliamali nchini wametakiwa kuongeza thamani bidhaa
wanazozizalisha pamoja na kuboresha vifungashio ,ili kuhimili
ushindani wa soko la ndani na nje ya nchi
Hayo yameelezwa na Meneja wa Sido Mkoani Arusha Linah Nchimbi katika
semina maalumu ya wanawake wajasiriamali iliyofanyika jijini Arusha na
kuandaliwa na kituo cha redio cha Arusha one FM kupitia mpango wao wa
Jipange Mwanamke 2019.
Meneja Huyo amesema kuwa bidhaa za wajasiliamali zinaweza kupata soko
kubwa iwapo zitaongezwa thamani na kufungashwa vizuri .
Meneja Miradi wa Radio Arusha One FM,Fredrick John Amesema kuwa
mpango huo unalenga kuwasaidia wajasiriamali wadogo ambao wamekua
wakijikwamua kwa kuwapa elimu ya masoko na jinsi ya kupanga bajeti.
Mratibu wa Mafunzo hayo ya Jipange Mwanamke 2019 ,Jamilah Mohammed
amesema kuwa wanatarajia kuwafikia wanawake wengi na kuwapa ujuzi wa kibiashara utakaoongeza thamani kwenye biashara zao.
Rukia Wiliam ambaye ni mjasiliamali anayejishulisha na uuzaji wa
vitafunwa aina ya vitumbua amesema kupitia biashara yake ndogo ameweza
kujenga nyumba nzuri ya kuisha na kwa sasa ana mpango wa kuanzisha
biashara nyingine hivyo maarifa hayo yatamuwezesha kukua kibiashara.
Mfanyabiashara anayeuza dagaa Advesta Christopher amesema kuwa
amehudhuria Mafunzo hayo ili kujua namna ya kuweka bajeti kuanzia
kwenye familia hadi kwenye biashara ili kukua kiuchumi .
Wajasiliamali wakiendelea na biashra ya bidhaa zao
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...