Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo Hussein Sayed,
akifurahia jambo na mshindi wa jumla wa Promosheni ya Chifu wa Mawakala Vicky
Ibrahim wakati akimkabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni
20 jijijini Dar es Salaam jana.
Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo Hussein Sayed,
(kushoto) akimkabidhi Said Khatibu (kulia)
ambaye ni mmoja kati wa mawakala watano wa Tigo Pesa watano walioibuka
washindi wa shilingi milioni 2 kutoka kanda ya Pwani katika Promosheni ya
mwisho wa mwaka 2018 inayojulikana kama Chifu wa Mawakala. Anayeshuhudia ni
Mkuu wa Bidhaa Tigo Pesa James Sumari.
Washindi wa Promosheni ya Chifu wa Mawakala
kutoka kanda ya Pwani wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa huduma ya
Tigo Pesa kutoka kampuni ya Tigo muda mfupi baada ya kukabidhi zawadi zao za
fedha taslimu.
Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo Hussein Sayed,
(kushoto) akimkabidhi Hajira Saidi(kulia)
ambaye ni mmoja kati wa mawakala watano wa Tigo Pesa watano walioibuka
washindi wa shilingi milioni 2 kutoka kanda ya Pwani katika Promosheni ya
mwisho wa mwaka 2018 inayojulikana kama Chifu wa Mawakala. Anayeshuhudia ni
Mkuu wa Bidhaa Tigo Pesa James Sumari.
Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo Hussein Sayed, (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) muda mfupi kabla ya kutoa zawadi za fedha taslimu kwa washindi kutoka kanda ya Pwani wa Promosheni ya mwisho wa mwaka inayojulikana kama Chifu wa Mawakala. Kulia ni Mkuu wa Bidhaa wa Tigo Pesa James Sumari.
Kampuni ya Tigo Tanzania, imetoa
zawadi ya fedha taslimu kwa mawakala wake wa Tigo Pesa waliofanya vizuri katika
promosheni ya mwisho wa mwaka 2018 inayojulikana kama “Wakala Chief Promotion”.
Kupitia promosheni hiyo, wakala aliyefanya vizuri kuliko wote nchini,
amepokea zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni 20 wakati mawakala wengine
wanaofuatia kwa kufanya vizuri kutoka kanda nne wakipokea jumla ya shilingi milioni
40.
Akiongea wakati wa hafla fupi ya kuwakabidhi washindi zawadi zao, Mkuu
wa Huduma za Kifedha wa Tigo Hussein Sayed alisema promosheni hiyo imewekwa
maalum kwa ajili ya kuwashukuru na kuwazadia mawakala wanaofanya vizuri katika
kipindi cha mwisho wa mwaka.
Hussein alisema, washindi 20 kutoka kanda nne ambazo ni Pwani, Kusini,
Kaskazini na Kanda ya Ziwa walipatikana ambapo kila kanda ilitoa washindi
watano ambao kila mmoja alijinyakulia zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni
mbili wakati mshindi wa jumla akiondoka na shilingi milioni 20.
“Jumla ya mawakala 90,000 walishiriki katika promosheni hii ya nchi
zima iliyoanza tarehe 1 Disemba na kumalizika tarehe 31 Disemba 2018,” alisema
Kwa upande wake Mkuu wa Bidhaa Huduma za Kifedha kwa njia ya Simu,
James Sumari aliongeza kwa kuwashukuru Mawakala kwa mchango wao mkubwa katika
kufikisha huduma za kifedha kwa wantanzania
“Tunayofuraha kutoa mchango unaowezesha wananchi wengi kufikiwa na
huduma za kifedha. Kupitia huduma ya Tigo Pesa, tumewawezesha mamilioni ya
Watanzania kutuma na kupokea fedha na kufanya malipo mbali mbali kwa urahisi na
kwa usalama. Tigo Pesa ni zaidi ya suluhisho kwa malipo na huduma rahisi za
kifedha, ni sehemu ya maisha,” alisema Sumari.
Vicky Ibrahim ambaye ni mshindi mkubwa katika
promosheni hiyo kutoka Kanda ya Pwani mkoa wa Dar es Salaam alisema, shilingi
milioni 20 alizojishindia zitamsaidia kupanua biashara yake hiyo ya Tigo Pesa
huku akiishukuru kampuni ya Tigo kwa zawadi hiyo.
“Ninayo furaha kubwa kupokea zawadi hii ambayo
kimsingi sikuitarajia. Nitatumia fedha hizi kupanua biashara yangu na kutatua
matatizo yangu binafsi ambayo yanahitaji fedha,” alisema.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...