NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa jimbo la mkuranga Abdalah Hamis Ulega ametoa mafuta ya diesel Lita 1000 kwa ajili ya greda ambalo husaidia kutatua changamoto za barabara jimboni humo pamoja na shuka 100 kwa kwa ajili ya hospitali ya Wilaya ya Mkuranga.
Akizungumza katika mkutano wa kufunga mwaka wa kutathimini changamoto na maendeleo uliofanyika wilayani humo, Ulega amesema kuwa ameamua kuchangia Mafuta,changamoto iliyotokana na Halmashauri kununua greda muda mrefu lakini limekaa bila kufanya kazi kwa kukosa Mafuta.
"Nilitoa msukumo kwa kukaa pamoja na madiwani na kushauriana kwa pamoja tuwe na greda letu wenyewe ili itusaidie kutatua changamoto za barabara hasa za vijijini ambako barabara nyingi hazipitiki na tumenunua greda hilo kwa zaidi ya milioni 700 ikiwa ni fedha zetu wenyewe na likachonge barabara zetu." Amesema Ulega.
Ulega amesema kuwa greda hilo halikodishwi kwa wananchi, ila kinachotakiwa vijiji vijichangishe vyenyewe kununua mafuta kwa shughuli za kutatua kero za barabara. "Sio kwamba nimeshindwa kutoa hela Mkurugenzi hela nakukabidhi mapipa haya matano ya mafuta kila moja lina Lita 200 yakatumike ipasavyo."Amesema Ulega.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akikabidhi shuka 100 kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkuranga, Mhandisi Mshamu Munde zenye thamani zaidi ya milioni moja,kushoto ni Mganga Mkuu wa wilaya ya
Mkuranga, Dkt.Stephen Mwandembo
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akimsikiliza Mzee Athuman Mtalu katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mkuranga mkoani Pwani.
Mkurugenzi wa Halmashauri Mkuranga, Mshamu Munde akizungumza na wananchi katika mkutano wa kufunga mwaka wa kutathimini changamoto na maendeleo uliofanyika wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mkuranga,Mh.Abdallah Ulega
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...