NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA VIJIJINI 

ZAHANATI ya Disunyara, kata ya Kilangalanga Kibaha Vijijini, inakabiliwa na ukosefu wa maabara hali inayosababisha kufuata vipimo ikiwemo cha malaria na damu kituo cha afya Mlandizi ambako kuna umbali wa km kumi kwenda na kurudi na nauli ya pikipiki sh. 4,000.

Kutokana na hali hiyo wakazi wa eneo hilo wamejitolea kuanza ujenzi wa maabara ambapo mbunge wa viti maalum mkoani Pwani, Subira Mgalu amechangia mifuko 30 ya saruji . 
 
Akichangia mifuko hiyo,alisema vipimo ni suala muhimu ambalo inahitajika nguvu ya pamoja kumaliza ujenzi huo. “Baada ya kusikia wananchi wameanza juhudi hizo ndipo nilipoguswa kuwaunga mkono ili kuendelea na ujenzi,alielezea Subira. 

Nae diwani wa kata hiyo, Mwajuma Denge alisema wananchi wanapata shida kufuata huduma ya vipimo umbali mrefu. Aliwaomba wadau kuendelea kujitokeza kuchangia ili kumaliza ujenzi huo waweze kupata japo vipimo vya awali karibu. Kwa upande wake mganga mfawidhi wa zahanati ya Disunyara ,Maimuna Yusuph alitaja tatizo la ukosefu wa chumba cha maabara kunasababisha akinamama wajawazito kwenda Mlandizi kufuata vipimo na wakati mwingine hushindwa kutokana na ukosefu wa nauli. 


Tatizo jingine ni vitanda vya kuzalia kwani kilichopo ni kimoja, kingine kibovu hivyo mahitaji ni vitanda vingine viwili ili kukidhi mahitaji. Mkazi wa Disunyara Mwajuma Juma alimshukuru Subira kwa kuwashika mkono ili kumkomboa mwanamke. Alisema endapo maabara hiyo ikikamilika itasaidia wakazi wenye mahitaji ya vipimo hasa akinamama na watoto.

Mbunge viti maalum mkoani Pwani, Subira Mgalu akizungumza wakati alipokwenda kutembelea zahanati ya Disunyara, huko Kibaha Vijijini. (picha na Mwamvua Mwinyi) .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...