Na Peter Haule, WFM, Kondoa

WANAFUNZI wote 3,287 waliochaguliwa kujiunga Kidato cha Kwanza katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma, wanatarajia kuanza masomo baada ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wa Jimbo la Kondoa, Dkt. Ashatu Kijaji, kutoa msaada wa mabati 1080 ya kuezekea vyumba 20 vya madarasa.

Akikabidhi msaada huo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Bw. Mustapha Semwaiko, Dkt. Ashatu Kijaji, amesema kuwa kipaumbele chake kikubwa ni elimu na anataka kila mwanafunzi aliyefaulu na kuchaguliwa kuendelea na masomo anapata fursa hiyo ya kusoma.

"Tumeamua kutumia mfuko wa Jimbo, zaidi ya sh. 20m zimetumika kununulia mabati haya na niombe Mkurugenzi wewe ndiye mwenye watendaji mpaka ngazi ya vijiji na vitongoji ambako shule zetu zipo, mabati haya yafikishwe kwenye kila shule ili inapofika mwisho wa mwezi Februari, 2019, watoto wote waanze kusoma" alisema Dkt. Kijaji

Aidha, Dkt. Kijaji amewapongeza viongozi na wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa kwa jitihada zao za kukuza elimu na kufanikisha Wilaya hiyo kufanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba mwaka 2018 ambapo shule nane kati ya kumi zilizofanya vizuri katika Mkoa wa Dodoma, zinatoka Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa.

"Tunakwenda kwenye Tanzania ya Viwanda, hatuwezi kuwapeleka wanaKondoa wasio na elimu ndio maana tumefanya mapinduzi makubwa katika wilaya yetu kutoka kuwa ya mwisho kielimu katika Mkoa wa Dodoma miaka mitatu iliyopita hadi kuwa na shule 8 zilizofanya vizuri kati ya 10, kimkoa" aliongeza Dkt. Kijaji

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Bw. Mustapha Semwaiko na Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya wilaya hiyo Bi. Hildegard Saganda, wamesema kuwa msaada huo umekuja wakati muafaka baada ya kuwa na wasiwasi wa namna ya kuwawezesha zaidi ya wanafunzi elfu 3 kupata nafasi ya kuingia kidato cha kwanza kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa uliokuwa ukiikabili Halmashauri ya Wilaya hiyo.

"Mbati haya yatapelekwa kwenye shule ambazo wananchi wamejenga maboma na zimefikia hatua ya lenta ambazo ni Busi, Kikore, Changaa, Kalamba, Itaswi, Kwadelo, Hondomairo na Loo" alifafanua Bi. Hildegard Saganda

Kwa Upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kondoa, ameelezea kuridhishwa kwake na namna Ilani ya CCM inavyotekelezwa katika wilaya yake katika nyanja mbalimbali na kumpongeza Dkt. Ashatu Kijaji kwa jitihada zake za kuiletea Maendeleo wilaya hiyo.
Afisa Elimu Sekondari wa Hamashauri ya Wilaya ya Kondoa, Bi. Hildegard Saganda, akisoma taarifa ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, muda mfupi kabla Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mbunge wa Jimbo la Kondoa, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, kabla ya kukabidhi mabati 1080 yenye thamani ya Sh. milioni 20 yatakayotumika kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 20 kwa ajili ya wanafunzi wa Kidato cha Kwanza.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kondoa Bw. Alhaji Othman Gora, akizungumza jambo wakati Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mbunge wa Jimbo la Kondoa, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji alipokabidhi mabati 1080 yenye thamani ya Sh. milioni 20 yatakayotumika kukamilisha vyumba vya madarasa 20 kwa ajili ya wanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika Halmashauri ya Wilaya hiyo. Kulia ni Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb).
Mabati 1080 yenye thamani ya Sh. milioni 20 yaliyokabidhiwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, yatakayotumika kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 20 kwa ajili ya wanafunzi wa Kidato cha Kwanza takribani 3287 waliofaulu katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa ambapo kati ya Shule za Msingi kumi bora zilizoongoza kwa ufaulu Mkoani Dodoma kwenye mtihani wa darasa la saba, shule nane zinatoka katika Halmashauri hiyo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mbunge wa Jimbo la Kondoa, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, akieleza umuhimu wa kuweka kipaumbele katika elimu kwa ujenzi wa taifa wakati akikabidhi mabati 1080 yenye thamani ya Sh. milioni 20 yatakayotumika kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 20 kwa ajili ya wanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa.
Naibu Waziri Wizara ya Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kulia), akimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Bw. Mustapha Semwaiko (wa pili kushoto), mabati 1080 yenye thamani ya Sh. milioni 20 yatakayotumika kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 20 kwa ajili ya wanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa.
Maafisa wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, wakishuhudia kukabidhwa mabati 1080 yenye thamani ya Sh. milioni 20 yatakayotumika kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 20 kwa ajili ya wanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa.
Mkurugenzi wa Wilaya ya Kondoa Bw. Mustapha Semwaiko, akimshukuru Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (hayupo pichani) baada ya kukabidhi mabati 1080 yenye thamani ya Sh. milioni 20 yatakayotumika kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 20 kwa ajili ya wanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa.
Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa tatu kulia) pamoja na viongozi na maafisa wa Halmashjauri ya Wilaya ya Kondoa wakizungumza jambo baada ya hafla ya kukabidhi mabati 1080 yenye thamani ya Sh. milioni 20 yatakayotumika kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 20 kwa ajili ya wanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa.(Picha na Peter Haule- Wizara ya Fedha na Mipango).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...