Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songea
Wakala wa
Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) pamoja na Bodi ya Nafaka na Mazao
Mchanganyiko zimetakiwa kuandaa mikakati ya haraka kuanisha jinsi watakavyo
nunua mazao ya wakulima nchini.
Wakati NFRA
imetakiwa kuainisha namna ya kununua nafaka za wakulima kwa upande wa Bodi ya
Nafaka na Mazao mchanganyiko yenyewe imetakiwa kujikita katika ununuzi wa mazao
mbalimbali ya wakulima ikiwa ni pamoja na kutafuta masoko ya mazao ndani na nje
ya nchi.
Kauli hiyo
imetolewa jana tarehe 5 Januari 2019 na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga (Mb), wakati akizungumza na wafanyakazi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya
Taifa ya Chakula (NFRA) mara baada ya kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa
maghala na vihenge vya kisasa.
Alisema
kuwa Wizara yake imekuwa ikihamasisha wakulima nchini kuzalisha kwa wingi mazao
kwa ajili ya chakula na biashara lakini inapofika hatua ya kuuza bei zinakuwa ndogo
jambo ambalo serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe
Magufuli haitalifumbia macho kamwe.
Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga (Mb),
akikagua ujenzi vihenge vya kisasa (Silos) na maghala ya kuhifadhia
nafaka kabla ya kuzungumza na wafanyakazi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi
ya Taifa ya Chakula (NFRA) Kanda ya Songea Mkoani Ruvuma, tarehe 5
Januari 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songea).
Waziri
wa Kilimo, Japhet Hasunga (Mb), akikagua hatua iliyofikiwa ya ujenzi
wa Vihenge vya kisasa (Silos) na maghala ya kuhifadhia nafaka kabla ya
kuzungumza na wafanyakazi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Taifa ya
Chakula (NFRA) Kanda ya Songea Mkoani Ruvuma, tarehe 5 Januari 2019.
Muonekano
wa hatua zilizofikiwa za mradi wa ujenzi wa Vihenge vya kisasa (Silos)
na maghala ya kuhifadhia nafaka umaojengwa na Wakala wa Taifa wa
Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) Kanda ya Songea Mkoani Ruvuma, tarehe 5 Januari 2019.
Waziri
wa Kilimo, Japhet Hasunga (Mb), akikagua ujenzi vihenge vya kisasa
(Silos) na maghala ya kuhifadhia nafaka kabla ya kuzungumza na
wafanyakazi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA)
Kanda ya Songea Mkoani Ruvuma, tarehe 5 Januari 2019.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...