Benki ya CRDB imekanusha taarifa zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii kuwa imefunga tawi lake la Chato kutokana na kukosa biashara.
Akizungumza na Globu ya Jamii jioni hii, Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa amesema kuwa taarifa hizo si za ukweli kwani tawi hilo linaendelea vyema na biashara na ni moja ya matawi yaliyofanya vizuri zaidi katika kipindi cha mwaka wa fedha uliopita.
"Tumeshangazwa sana na taarifa hizi kwani hata ukiangalia taarifa yenyewe haina ubora unaoendana na taaluma yetu. Mimi ndiye mhusika mkuu wa kutoa matangazo yote kwenye magazeti na vyombo vyote vya habari, Naomba kusema kuwa silitambui tangazo hilo”.
Aliendelea kusema “Nichukue fursa hii kuwatangazia wateja wetu na Watanzania wote kwa ujumla kuwa Benki ya CRDB haijafunya na wala haina mpango wa kufunga tawi lolote nchini" kiukweli, benki ya CRDB iko katika mkakati kabambe wa kutanua wigo wa utoaji huduma zake kwa kutumia ubunifu na teknolojia ili kuwafikia watanzania wengi vijijini kupitia uwakala. Mwaka huu tunataka kuongeza mawakala zaidi ya 10,000”. alisema Bi. Mwambapa

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...