Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma Sophia Mfaume Kizigo ameiomba mahakama kutoa huduma ya sheria kwa wananchi kizalendo.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Sheria wilayani humo jana katika uwanja wa Taifa mjini Namtumbo Mkuu wa wilaya huyo aliwataka wanasheria kutenda haki katika kuzingatia uzalendo katika nchi yao.

Aidha Mkuu wa wilaya huyo alidai yapo malalamiko machache kuhusu kukilalamikia chombo hicho cha mahakama katika ofisi yake hali inayoonesha sehemu kubwa ya chombo hicho kinatenda haki alisema mkuu wa wilaya huyo.

Hata hivyo aliwataka wananchi wilayani hapa kukitumia chombo hicho cha mahakama kuwafikisha wahalifu wanaoweka mimba wanafunzi badala ya wazazi kuendesha mashauri ya mimba majumbani na kumaliziana kinyumbani huku wanafunzi wa kike wakikosa haki yao ya msingi ya kupata elimu.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wilaya ya Namtumbo Bi. Gloria Lwomile alimwambia Mkuu wa wilaya changamoto ya kucheleweshwa kwa upelelezi kutoka jeshi la polisi husababisha kesi nyingi kuchukua muda mrefu pamoja na changamoto ya uchache wa watumishi wa mahakama wilayani humo.

Lwomile alidai mahitaji ya watumishi wilayani humo ni mahakimu 2 katika mahakama ya mwanzo na aliopo ni mmoja na pia katika mahakama ya wilaya mahitaji ya mahakimu ni watumishi 9 na waliopo ni watumishi 7.

Iddi Chowo mkazi wa Namtumbo alisema maadhimisho ya siku ya sheria yameweza kumwongezea ufahamu hasa katika swala la kumwekea mtu dhamana haihitajiki kutoa fedha bali kinachohitajika ni kukamilisha taratibu za kumwekea mtu dhamana alisema bwana chowo.

Kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria wilayani Namtumbo yalifanyika katika kiwanja cha Taifa mjini Namtumbo ambapo awali yalitanguliwa na utoaji elimu kwa wananchi kuhusu kufahamu mambo ya sheria.

 Picha ya kwanza inaonesha Mkuu wa wilaya Namtumbo akiwa katika picha ya pamoja na wanasheria mara baada ya kumaliza kuadhimisha siku ya sheria wilayani Namtumbo ambapo waliaswa kutumia taaluma zao kutenda haki kwa wananchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...