MKuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli (TRC)Bw. Masanja Kadogosa wakati alipowasili tayari kwa kuongoza wasanii na waandishi wa habari kwa ajili ya kutembelea na kujionea namna shughuli za ujenzi wa reli ya kisasa ya umeme Starndard Gauge Railway (SGR) kutoka Dar es salaam kwenda Morogoro unavyoendelea, ambapo treni hiyo imeondoka leo na wasanii wa fani mbalimbali pamoja na wanahabari wa vyombo mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii. (PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE)
MKuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akizungumza jambo kabla ya kukagua mradi huo eneo la kamata na kisha kuanza safari na waandishi wa habari pamoja na wasanii mbalimbali jijini Dar es salaam kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Reli (TRC) Bw. Masanja Kadogosa. 
MKuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akifanya ukaguzi mdogo wamradi huo eneo la kamata kabla ya kuondoka na msafara huo kushoto ni Mkurugenzi wa TRC Bw. Masanja Kadogosa na kulia ni Steve Nyerere Mratibu wa ziara hiyo. 
MKuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa TRC Bw. Masanja Kadogosa wakati akifanya ukaguzi mdogo wa mradi huo eneo la Kamata kabla ya kuondoka na msafara huo kushoto ni Steve Nyerere Mratibu wa ziara hiyo. 
Mafundi wa kampuni ya Yapi Merkezi wakiendelea na kazi ya kujenga nguzo. 
Meneja wa WCB Babu Tale na Promota wa ngumi Bw. Kaike ni miongoni mwa watu waliojiambatana na wasanii wengine katika ziara hiyo 
Wasanii Peter Msechu na Mrisho Mpoto wakiwa katika ziara hiyo pia. 
Picha zikionyesha wasanii mbalimbai ambao wapo katika ziara hiyo kabla ya kupanda treni na kuanza safari ya kwenda Morogoro. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...