Uchambuzi Madhubuti katika kuielewa Sanaa ya Yoga na mafunzo yake, haina budi pia kuzielewa na kutambua faida zake kimifano kupitia wahusuka na mchezo huo wa Sanaa isiyo ya kawaida kwa wengi. Ipo mifano mingi sana katika sehemu tofauti ambako mafunzo haya ya Yoga yametumika kama utafiti kuwezalinganisha tabia na stahimili za kujenga uvumilivu na kuwa na upeo wa kuyaona mengi kifikra na kuyatafakari kabla ya maamuzi yoyote ili kuepuka maamuzi yasio stahili na kuleta madhara.
Mfano wa kwanza, Canada, ni nchi iliyoendelea na
imefanya utafiti mkubwa katika jeshi lake la polisi kwa kuwahusisha baadhi ya
maofisa wake katika kozi ya Yoga na kutafakari kabla ya kuanza kazi kila siku
ili kutuliza mawazo na kuwa na utulivu wa kuwamuda raia wake wakati wa shughuli
zao za dolia ( https://www.reddit.com/.../canadian_polic.. ), (https://www.canadaamindfulnation.ca/.../).
Kwani, nchi ya jirani na Canada, Marekani, hivi karibuni mnamo miaka michache
iliyopita, imebainika kwamba maafisa wa jeshi la Marekani hutumia nguvu nyingi
sana zisizohitajika katika kuwa kabili wa harifu au watuhumiwa kutokana na kile
kiitwacho hasira au chuki za ubaguzi nchini humo. Hiyo ndio moja ya sababu kuu
nchini Canada polisi hawana lawama kama zile za wenzao wa Marekani. Na sababu
kubwa ni kile kiitwacho amani na ustamilivu wa fikra na utumiaji wa nguvu au
unyanyasaji wa haki za raia.
Mfano wa pili
ni wafungwa huko nchini New Zealand (https://www.yogainprisonstrust.org/), na mwisho ulifanyika nchini Afrika Kusini ( South
Africa) 2016 (https://www.pressreader.com/south-africa..). Kutokana na vurugu
na ukatili wa wafungwa wa jela za ulinzi wa usalama wa hali ya juu wa huko
Afrika ya Kusini, utafiti huo wenye lengo la kujaribu kama kweli mafunzo ya
Yoga yatawasaidia wafungwa hao kuwa wapole na utulivu wa mawazo na fikra
ilikupunguza ghasia na fujo ndani ya jela hizo. Matokea yake ni kwamba
ilibainika kuwa asilimia 90 za washiriki na hali ya jela ilikuwa shwari na fujo
zilitulia n ahata wengi wa wafungwa hao walibadilika na kuwa na tabia njema na
kuwa na utulivu sababu mafunzo hayo yamewezesha kuilekez mihimili ya mawazo yao
katika njia sahihi kimawazo kupitia mafunzo haya ya Yoga.
Faida kuu za mafunzo haya kwa mifano na ushahidi
toka kwa washiriki mbalimbali wa mafunzo haya ni : kulainisha viungo, kupunguza
shinikizo la damu, utulivu wa fikra na mawazo, kupunguza “stress”; maumivu ya kichwa,
mgongo, na viungo au mifupa. Zipo faida
na vyakula muhimu katika kulifanikisha zoezi hili la afya ya mwili na fikra
liwe na faida bora katika Maisha ya mtu wa kawaida. Leo hii, katika nchi za
viwanda na zilizoendelea, watu wengi wana badilisha mfumo mzima wa maisha yao
baada ya kuwa na mambo yanayochangia
hatarisha afya zao, ikiwemo vyakula, ulevi kupita kiasi na uvutaji sigara.
Mtaalam wa somo hili la Yoga bwana Rumadha Fundi,
alisoma kozi hii chini ya tawi la chama cha Yoga cha mjini Tiljala, Kolkata,
India, katika tawi la chuo hicho (European Bracnh) College of Neo Humanist Studies, Gullringen, Vimmaby, Sweden 1985
hadi 1987 na kupata Diploma ya Yoga.
Hatimae kwenda India kwa mafunzo ya mwisho baada ya miaka miwili ya mafunzo ya
awali huko Sweden.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...