Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
MEYA
wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam Abdallah Chaurembo ametoa
ombi kwa Benki ya Dunia kuendelea kuisaidia fedha Serikali ya Tanzania
na hasa ndani ya manispaa hiyo ili kuendelea kutekeleza miradi ya
maendeleo ya wananchi.
Chaurembo
ametoa ombi hilo wakati maofisa wa Benki ya Dunia walipofanya ziara ya
kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo kupitia Mradi
wa Utekelezaji wa Jijii la Dar es Salaam (DMDP).
Maofisa
hao wa benki ya dunia wametembelea miradi hiyo wakiongozwa na Waziri wa
Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)
Sulemani Jafo.
Akifafanua
zaidi kuhusu utekelezaji wa miradi ya DMDP ,Chaurembo amesema katika
kufanikisha miradi hiyo wao Temeke waliamua kukopa fedha Benki ya CRDB
Sh.Bilioni 20 ambazo zilitumika kulipa fidia wananchi katika baadhi ya
maeneo ili kupisha mradi huo.
Ameongeza
kwa kumwambia Waziri Jafo kuwa pamoja na kukopa fedha hizo wameendelea
kulipa deni bila tatizo na manispaa ya Temeke iko salama kwani
utekelezaji wa miradi ya maendeleo unakwenda vizuri.
"
Pamoja na kukopa fedha Sh Bilioni 20 kutoka Benki ya CRDB ,tunalipa
deni bila tatizo.Pia tunaendelea na kutekeleza miradi mbalimbali ndani
ya manispaa yetu.Hivyo Temeke tuko salama sana,"amesema Chaurembo.
Pia
amesema wanatoa ombi kwa Serikali ili kupata fedha hizo za fidia kama
ambavyo imefanyika kwa manispaa ya Kinondoni na Ilala,hivyo ni vema
Serikali Kuu ikawapa fedha hizo.
Wakati
huo huo ametumia fursa hiyo kutoa ombi kwa Benki ya Dunia iwapo bajeti
yao itaruhusu waendelee kuisaidia fedha Manispaa ya Temeke na kufafanua
kuwa mrado wa DMDP unatekelezwa katika kata 12 na hivyo bado kuna kata
nyingine ambazo nazo zinahitaji kuendelezwa.
"Tunashukuru
Serikali yetu ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk.John Magufuli ambaye
amedhamiria kuboresha maisha ya wananchi kupitia miradi ya maendeleo.
"Kwetu
Temeke pamoja na kutambua juhudi hizo tunaomba ombi kwa Benki ya Dunia
kuendelea kutusaidia fedha kwa kushirikiana na Serikali yetu ili
tuendelee kuboresha maeneo yetu," amefafanua Chaurembo.
Kuhusu
namna ambavyo miradi inavyotekelezwa,Chaurembo amesema viongozi wa
Manispaa ya Temeke wakiwamo madiwani wamekuwa makini kuhakikisha thamani
ya fedha inayotolewa kwa ajili ya miradi hiyo inakwenda sambamba na
ubora wa mradi.
"Tumekuwa
makini kufuatilia miradi hii ili iandane na fedha inayotolewa.Ndio
maana miradi hii kwa Temeke inavutia sana na inatekelezwa kwa kiwango
cha hali ya juu," amesema Chaurembo huku akisisitiza kwa usimamizi mzuri
wa miradi hiyo ndio maana wanapata ujasiri wa kuomba fedha kwa ajili ya
kuendelea kuboresha miundombinu.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...