Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema kifo cha mmoja wa waasisi na Mkurugenzi wa Vipindi
na Uzalishaji wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba ni pigo kubwa kwa Serikali kwani enzi za
uhai wake ametoa mchango mkubwa kuhakikisha maono ya viongozi yanapata fursa ya
kutekelezwa kwa vitendo.
Majaliwa amesema hayo leo Februari 27 , nyumbani kwa wazazi wake Ruge jijini Dar es Salaam
wakati anatoa salamu za Serikali kutokana na kifo hicho ambapo amesema ni pigo kwa familia
na zaidi ni pigo kwa Serikali.
"Nimekuja hapa nyumbani kutoa salamu za pole kwa wazazi, familia, watoto, ndugu, jamii,
marafiki na Watanzania wote kwa kuondokewa na Ruge Mutahaba.Kifo chake ni pigo kubwa
kwa Serikali kwa nyakati tofauti tulikuwa tunashirikiana naye.Alikuwa mstari wa mbele
kuhamasisha vijana kuipenda nchi yao kwa vitendo.
"Ruge alitumia akili na aina ya maarifa yake kwa ajili ya kusaidia wengine, aliwahimiza vijana
kufanya kazi kwa bidii. Alisisimama imara kufanikisha falsafa za viongozi wakuu wa nchini
kuanzia Rais mstaafu Dk.Jakaya Kikwete na Rais wetu Dk.John Magufuli kuhakikisha vijana
wanatumia fursa zilizopo nchini kufanya maendeleo. Tunaamini Ruge alikuwa ni kiongozi wa
vijana wengine nchini,"amesema Waziri Mkuu.
Amefafanua kwamba wakati wote na kwa nyakati tofauti Watanzania walikuwa wakimuombea
ili Ruge apate nafuu lakini ukweli leo hii hatunaye tena na kubwa zaidi ni kuendelea kumuombea
kwa Mwenyezi Mungu ampe pumziko la milele.
"Nirudie tena kifo cha Ruge ni pigo kubwa , alitumia fedha na mali zake kwa ajili ya kuwasaidia
Watanzania na amefanya mambo makubwa sana na ameshiriki kwa vitendo katika harakati za
maendeleo ndani ya nchi yetu.Ruge amezunguka nchi nzima kupitia kampeni mbalimbali
kuelezea umuhimu wa vijana kutambua nchi yao na kuwajengea uelewa wa kufanya mambo
makubwa, "amesema Waziri Mkuu.
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi 'ubani wa msiba' Baba wa Marehemu Prof Mutahaba,alipokwenda kuhani msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba kwa niaba ya Serikali, nyumbani kwa wazazi wa marehemu Mikocheni jijini Dar es Salaam.
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi 'ubani wa msiba' Baba wa Marehemu Prof Mutahaba,alipokwenda kuhani msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba kwa niaba ya Serikali, nyumbani kwa wazazi wa marehemu Mikocheni jijini Dar es Salaam.
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza mbele ya waandishi wa habari mapema leo alipokwenda kuhani msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba kwa niaba ya Serikali, nyumbani kwa wazazi wa marehemu Mikocheni jijini Dar es Salaam.
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa akiwasalimia baadhi ya viongozi waliofika kuhani msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba kwa niaba ya Serikali, nyumbani kwa wazazi wa marehemu Mikocheni jijini Dar es Salaam.
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Clouds Media Group,Joseph Kusaga ,alipokwenda alipokwenda kuhani msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba kwa niaba ya Serikali, nyumbani kwa wazazi wa marehemu Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...