Wafanyakazi wa kiwanda cha Global Packaging (T) Ltd cha Kibaha mkoani Pwani wakiendelea na kazi ya kuzalisha vifungashio vya aina mbalimbali. Kiwanda hicho kinazalisha tani 150 za vifungashio kwa mwezi na kutoa ajira kwa mamia ya watanzania na pia kuondoa changamoto ya upatikanaji wa vifungashio hapa nchini.

Mitambo ya wa kiwanda cha Global Packaging (T) Ltd cha Kibaha mkoani Pwani kama inavyoonekana katika picha, hiki ni moja ya kiwanda kinachozalisha vifungashio hapa nchini ikiwa ni matokeo ya dhana ya ujenzi wa uchumi wa viwanda inayosisistizwa na Serikali ya Awamu ya Tano.
Wafanyakazi wa kiwanda cha Global Packaging (T) Ltd cha Kibaha mkoani Pwani wakiendelea na kazi ya uzalishaji vifungashio kwa kutumia mitambo ya kisasa. Kiwanda hicho kinazalisha tani 150 za vifungashio kwa mwezi na kutoa ajira kwa mamia ya watanzania na pia kuondoa changamoto ya upatikanaji wa vifungashio hapa nchini.


Sehemu ya mitambo ya kuzalisha vifungashio katika Kiwanda cha Global Packaging (T) Ltd cha Kibaha mkoani Pwani.
(Picha zote na MAELEZO)


Na Lilian Lundo – MAELEZO


Kiwanda cha Global Packaging (T) Limited kilichopo Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Mkoa wa Pwani kimepunguza kwa kiasi kikubwa uagizaji wa vifungashio nje ya nchi.

Hayo yameelezwa mapema wiki hii na Meneja Mradi wa kiwanda hicho, Hatibu Njuwila wakati wa mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii.“Kiwanda kilianza uzalishaji Januari, 2017 na kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli , kinazalisha tani 150 za mifuko au vifungashio kwa mwezi,” amesema Njuwila.

Ameendelea kusema, wateja wakubwa wa kiwanda hicho ni wakulima wanaozalisha bidhaa za nafaka kama vile mahindi, mtama na mchele, bidhaa zinazotokana na madini na mazao mengine yanayohitaji vifungashio.Amesema, lengo la uanzishwaji wa kiwanda hicho ni kupunguza uagizaji wa vifungashio nje ya nchi kutokana na kuwepo na uigizaji mkubwa wa vifungashio kutoka nje ya nchi kwa gharama kubwa.

Aidha amesema, mafanikio waliyoyapata katika kipindi cha miaka miwili tangu kuanza kwa uzalishaji wa kiwanda hicho ni pamoja na kuajili wafanyakazi 98 ambao wote ni Watanzania, ambapo kwa asilimia kubwa ni kutoka Halmashauri ya Kibaha.Mafanikio mengine ni kupunguza kwa kiasi kikubwa uagizaji wa vifungashio kutoka nje ya nchi, kulipa kodi mbalimbali za Serikali Kuu pamoja na Halmashauri ambapo imeongezea Serikali mapato.

Matarajio ya kiwanda hicho ni kuzalisha vifungashio vyenye ubora na ambavyo vinakidhi mahitaji ya wateja ambayo itaongeza thamani ya mazao na uhifadhi na kupata masoko ya uhakika ndani na nje ya nchi.Global Packaging (T) Limited imejipanga vyema kutekeleza sera ya Serikali ya viwanda kwanza kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...