Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango(Mb) akifafanua hoja wakati wa mjadala wa Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali, uliowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Prof. Adelardus L. Kilangi, Bungeni Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani(Mb) wakijadili jambo kabla ya kuwasilishwa kwa Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali, Bungeni Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akijadiliana jambo na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani (Mb), bungeni Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango(Mb) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Prof. Adelardus L. Kilangi wakijadili jambo baada ya kuwasilishwa kwa Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali, bungeni Jijini Dodoma.


Na. Josephine Majura, WFM, Dodoma 

Bunge limepitisha Muswada wa Sheria wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba mbili ya Mwaka 2019 ambao umelenga kutatua changamoto za za kodi ikiwemokodi ya Majengo, madini na Kodi uya Ongezeko la Thamani (VAT). 

Muswada huo uliopelekwa Bungeni kwa Hati ya Dharura ulijadiliwa na kupitishwa ambapo Wabunge mbalimbali walipata fursa ya kutoa maoni yao. 

Akizungumza wakati wa kuwasilisha Muswada huo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Prof. Adelardus Kilangi, alisema kuwa marekebisho hayo yameondoa kodi ya zuio (withholding tax) kutoka 5% hadi asilimia sifuri kwenye bei ya kuuzia madini ya aina zote kwa wachimbaji wadogo ili kuwahamasisha wachimbaji hao kuuza madini katika masoko ya madini. 

Alisema marekebisho hayo yanalenga kudhibiti upotevu wa mapato ya Serikali na kuhakikisha mapato yanayotokana na biashara ya madini yanakusanywa ipasavyo. 

Aliongeza kuwa Muswada huo umependekeza kutoa msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa wachimbaji wadogo wa madini watakaouza madini yao katika masoko ya madini na vituo vya ununuzi wa madini. 

Aidha, Prof. Kilangi alibainisha kuwa Muswada huo pia umependekeza kila kiwanja kitozwe Kodi ya Majengo badala ya kila jengo lililopo ndani ya kiwanja husika kwa maeneo ya Halmashauri za Wilaya. 

Sheria zilizopitishwa ni pamoja nma Sheria ya Ushuru wa Bidhaa Sura ya 147, Sheria ya Kodi ya Mapato Sura ya 332, Sheria ya Mamlaka za Serikali za Mitaa ya Utozaji wa Kodi ya Majengo Sura ya 289, Sheria ya Madini Sura ya 123 na Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani Sura ya 148. 

“Madhumuni ya marekebisho ya Sheria hizo pamoja na mambo mengine ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya kuondoa changamoto kwa wachimbaji wadogo wa madini, wakulima wa zabibu ndani ya nchi na viwanda vinavyotumia zabibu hiyo katika uzalishaji pamoja na kuweka viwango mfuto (fixed rate) vya kodi ya majengo.” Alisema Prof. Kilangi. 

Alisema kuwa Serikali imeona upo umuhimu wa kuwasilisha Muswada huu kwa haraka kupitia Hati ya Dharura ili kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo kupunguza utoroshwaji wa madini nje ya nchi unaofanywa na wachimbaji wadogo ambao wanakwepa kodi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...