Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri amesema matukio ya utekaji na mauji ya watoto Wilayani Njombe yamesababisha uchumi kuzorota kwa kushuka kwa uzalishaji mali kwa wananchi.
Amesema hali hiyo inatokea kwa kuwa wazazi wanatumia muda mwingi kwapeleka watoto na kuwafuata watoto shule hivyo kupoteza muda na kusimamisha shuguli zao.
Ameyasema hayo jana wakati akifunga maombi katika Kanisa la TAG Milinze yaliyolenga kuombea Wilaya hiyo kuondokana na matukio ya utekaji na mauaji ya watoto.“ Hatuwezi kufikia uchumi wa Viwanda kama matukio haya yataendelea wazazi wanapoteza sana muda katika kuhakikisha watoto wao wanapata ulinzi kwa kuwapeleka na kuwarudisha nyumbani” amesema
“ Niwaambie tu Halmashauri ya Mji wa Njombe inaoongoza katika Halmashauri zote nchini kwa kuwa na kipato kikubwa ana kwa mwaka mwananchi wa hapa ana uwezo wa kuwa na shillingi million 5”
Mkuu wa Wilaya huyo amewataka waumini wa Kanisa hilo na wananchi wa Wilaya na Mkoa wa Njombe kwa ujumla kuombea mkoa wao ili kuondokana na vitendo hivyo vinavyopelekea kuzorotesha shughuli za kiuchumi.
Akitoa salama za Wizara Mwenyekiti wa Timu ya Wataalam kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara za Maendeleo na Ustawi wa Jamii) Bi. Hanifa Selengu amesema Serikali ipo pamoja na wananchi wa Mkoa wa Njombe katika kulaani matukio hayo ya utekeaji na mauaji ya watoto yaliyojitokeza.
Mkuu
wa Wilaya ya Njombe Mhe. Ruth Msafiri akizungumza na waumini wa Kanisa
la TAG Melinze wakati wa kufunga maombi ya kuuombea mkoa wa Njombe
kutokana na mauaji ya Watoto yaliyotokea Mkoani Njombe.
Mwenyekiti
wa Timu ya Wataalam kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto ( Idara za Maendeleo na Ustawi wa Jamii) Bi. Hanifa
Selengu akitoa salamu za Wizara kwa waumini wa Kanisa la TAG Melinze
wakati wa kufunga maombi ya kuuombea mkoa wa Njombe kutokana na mauaji
ya Watoto yaliyotokea Mkoani humo.
Waumini
wa Kanisa la TAG Melinze wakimsikiliza MKuu wa Wilaya ya Njombe Mhe.
Ruth Msafiri (hayuko pichani) wakati wa kufunga maombi ya kuuombea mkoa
wa Njombe kutokana na mauaji ya Watoto yaliyotokea Mkoani humo.
Mkuu
wa Wilaya ya Njombe Mhe. Ruth Msafiri (wa Tano kulia) akiwa katika
picha ya pamoja na Waumini wa Kanisa la TAG Melinze na Timu ya
Wataalam kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto ( Idara za Maendeleo na Ustawi wa Jamii mara baada ya kufunga
maombi ya kuuombea mkoa wa Njombe kutokana na mauaji ya Watoto
yaliyotokea Mkoani humo.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...