Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akizungumza na viongozi wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kuhusu madaktari kuimarisha mawasiliano na wagonjwa ili kuwapa fursa ya kujua mwendendo wa matibabu yao.
Baadhi ya wakurugenzi wa Muhimbili na JKCI wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Museru leo kuhusu uboreshaji wa huduma za matibabu kwa wagonjwa wanaotibwa katika taasisi hizo.
Baadhi ya wakurugenzi wa Muhimbili, MOI na Muhimbili-Mloganzila wakiwa kwenye mkutano huo leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Prof. Mohamed Janabi akichangia mada kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea leo katika ukumbi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo. 



Viongozi wa taasisi nne; Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila zimekutana leo kujadiliana jinsi ya kuboresha huduma za matibabu kwa wagonjwa wanaotibiwa katika taasisi hizo.

Katika mkutano huo, wakurugenzi na wakuu wa idara wamekubaliana kuimarisha mawasiliano katika taasisi hizo ili kuhakikisha wagonjwa wanaendelea kuonwa na wataalam kwa wakati.

Akizungumza na viongozi hao, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru ambaye amekuwa Mwenyekiti wa mkutano huo, amewaomba wakurugenzi wenzake kuendelea kuimarisha ushirikiano na kuandaa mikutano ya mara kwa mara baina ya taasisi hizo.

“Sisi kama wakurugenzi tuendelee kuwahimiza madaktari na watalaamu wengine kuimarisha mawasiliano yao na wagonjwa ili kuwapa fursa ya kujua mwendendo wa matibabu yao,” alisisitiza Prof. Museru.

Alisema uwepo wa mawasiliano mazuri baina ya watoa huduma na wananchi wanaohudumiwa utapunguza malalamiko yanayojitokeza mara kwa mara kuhusu mwenendo wa matibabu kwa wagonjwa.

Pia, katika mkutano huo, taasisi hizo zimekubaliana kutumia miundombinu iliyopo kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa endapo taasisi moja itakua imeelemewa.

“Kwa mfano, MOI au Muhimbili inaweza kulaza wagonjwa wa ICU wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa muda kama ICU yao imejaa huku wakisubiri kupata nafasi ya kitanda katika taasisi hiyo ya Moyo,” amesema Mkurugenzi huyo.

Taasisi hizo zitakuwa zikikutana mara kwa mara ili kujadiliana changamoto mbalimbali zinazojitokeza, huku lengo kubwa likiwa ni kuboresha huduma za matibabu zinazotolewa MNH, MOI, JKCI na Muhimbili- Mloganzila.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...