Wiki ya kutoa elimu na ushauri wa kisheria imezinduliwa katika Mkoa wa Shinyanga mapema leo tarehe 02/02/2019 huku watendaji wa Idara mbalimbali wakitakiwa kutenda haki kwa wananchi ili kupunguza malalamiko kwenye ofisi za Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amesema wananchi wengi wanakwenda kwenye Ofisi yake na Mkuu wa Wilaya kulalamika kuhusu kutokamilika kwa mashauri yao Mahakamani.
" Nimechoka kusikia Shinyanga ikizungumziwa kwa rushwa rushwa, watu wanakimbia mahakamani kwa sababubhawatendewi haki, wanakuja Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Wilaya ndiyo kwenye haki"
Mhe. Telack amesisitiza kuwa, hawezi kukaa akaangalia wananchi wakilalamika watumishi kuwataka rushwa ili kutekeleza majukumu yao.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe,. Zainab Telack akisaini kitabu cha wageni huku akipata maelekezo ya Afisa Huduma kwa jamii kutoka Idara ya huduma za uangalizi,Wizara ya mambo ya ndani, Bi Monica Dawa.

Mkuu w Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack, akielekea kwenye mabanda ya wadau wa sheria katika kuzindua wiki ya sheria Duniani, Mkoani Shinyanga mapema leo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Venant Mboneko.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...