KATIKA kukabiliana na changamoto ya utoaji wa huduma ya afya kwa wananchi, serikali ya awamu ya tano inajenga hospitali za wilaya tatu za kisasa , halmashauri ya Kibaha Mjini, Kibaha Vijijini na Kibiti mkoani Pwani ambazo zitagharimu kiasi cha sh. bilioni 4.5.
Akizungumza wakati alipotembelea ujenzi wa hospital ya halmashauri ya Mji wa Kibaha ,Lulanzi kata ya Pichandege, kwenye ziara yake inayoendelea kukagua miradi ya maendeleo, mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo alisema kukamilika kwa hospital hizo, kutaondoa kero ya kutembea umbali mrefu kufuata matibabu.
“Kila hospital inatarajiwa kugharimu bilioni 1.5 ,matarajio yetu ni kuona ujenzi unakamilika na sio kuanza mradi na kisha kusuasua “alieleza Ndikilo.
Aidha ameelezea, fedha zote zinazoelekezwa katika miradi hiyo muhimu zitumike kwa wakati na kwa matumizi lengwa bila kuziacha kubaki viporo.
Hata hivyo Ndikilo, aliwaasa wahandisi wa halmashauri ya Kibaha Mji na wa serikali ya mkoa huo kujiwekea utaratibu wa kutoka maofisi kwenda kutembelea miradi pasipo kusubiria ziara ama kiongozi kutembelea ndipo nao watoke maofisini.
Nae mkuu wa wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama alitoa rai kwa jamii kushirikiana na serikali katika kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya elimu na kujitolea kwenye miradi ya kimaendeleo.
Diwani wa kata ya Picha ya ndege Robert Machumbe alieleza, nia ya serikali ni kuwaletea wananchi mabadiliko chanya ya kimaendeleo ambapo amefafanua kwamba, eneo hilo linalojengwa hospital lina ukubwa wa hekari 25 lipo eneo linalojengwa shule ya sekondari Lulanzi lenye ukubwa wa hekari 11.7



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...