NA MWAMVUA MWINYI, PWANI
MKUU wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo, ametoa agizo kwa wakuu wa wilaya, maafisa tarafa na watendaji wa kata kuwasaka baadhi ya watoto wa wafugaji wenye umri wa kwenda shule za msingi na sekondari ambao hawajapelekwa shule hadi sasa na badala yake wakishinda kuchunga mifugo .
Aidha amewataka wakuu wa wilaya , wakurugenzi kwa kushirikiana na halmashauri kuhakikisha wanajenga madarasa 119 ili kuwawezesha wanafunzi 4,713 waliofaulu kidato cha kwanza mwaka jana na kukosa kuendelea na masomo kutokana na upungufu wa mdarasa hayo waweze kuanza masomo .
Akitoa maelekezo hayo wakati wa ziara yake ya kutembelea ujenzi wa vyumba vya madarasa ambayo aliyoianza mkoani Pwani, akiwa Bagamoyo mkuu huyo wa mkoa aliwaasa ,wazazi wao waache tabia ya kuwatumikisha watoto hao katika ufugaji na kuwasababishia kukosa elimu haki yao ya kielimu .
Alieleza, endapo watoto hao wakisakwa na kupelekwa shule itasaidia kupata elimu kwani ndio msingi wa maisha yao.
Akielezea suala la ujenzi wa miundombinu ya madarasa, Ndikilo alisema hadi kufikia January 31 mwaka huu wanafunzi walifaulu na kuripoti mashuleni ni 11,822 awamu ya kwanza ambapo wanafunzi 4,713 wameshindwa kutokana na ukosefu wa madarasa.
"Hadi sasa mkoa umepokea bilioni 12.9 kwa ajili ya elimu bila malipo, pamoja na bilioni 3.245 ya ujenzi wa miundombinu ya madarasa, kwa hivyo serikali wakati inafanya jitihada hizo na jamii tushirikiane kutatua kero zilizopo "alisisitiza Ndikilo.
Nae mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Zainab Kawawa alisema kuwa, Bagamoyo ina uhaba wa madarasa 22 hadi sasa baada ya ujenzi wa madarasa nne kuendelea kujengwa shule ya Mapinga sekondari .
Awali diwani wa Mapinga ,Ibrahim Mbonde alisema ,ujenzi wa madarasa manne shule ya sekondari ya kata Mapinga hadi sasa upo hatua ya gebo, umegharimu milioni 33,na hadi kukamilika utahitajika milioni 100.
Alisema kukamilika kwa ujenzi huo kutawezesha kupunguza msongamano shule ya sekondari Kerege ambayo inahemewa na wanafunzi ambao wengine wanatokea kata ya Mapinga.
Mkuu wa mkoa wa Pwani, ameanza ziara hiyo wilaya ya Bagamoyo kwa kukagua mradi wa ujenzi wa madarasa hayo manne, mradi wa kituo cha afya Matimbwa na mradi wa mfereji wa maji mtaa wa benki.
MKUU wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo, akitoa agizo kwa wakuu wa wilaya, maafisa tarafa na watendaji wa kata kuwasaka baadhi ya watoto wa wafugaji wenye umri wa kwenda shule za msingi na sekondari ambao hawajapelekwa shule hadi sasa na badala yake wakishinda kuchunga mifugo .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...