Mkurugenzi
wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dkt Hassan Abbas
akizungumza na waandishi habari wakati alipokwenda kutoa pole ya Msiba
wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji Vipindi wa Clouds Medio Group,Ruge Mutahaba
aliyefariki Jana nchini Afrika Kusini. Dkt Abbas amesema Ruge alikuwa
kijana wa pekee aliyetoa mchango wake ambao umeweza kuonekana katika
kusaidia vijana wengi nchini.Amesema kuwa vijana waliobaki nao waoneshe
njia zilizoachwa na Ruge kwa kuamini katika kusaidia wengine. Amesema
Ruge ametutoka lakini tulikuwa na muhitaji lakini kazi ya Mungu haina
makosa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...