Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

Serikali imesema kuwa katika kuelekea uchumi wa viwanda kunahitaji kuwekeza nguvu kwa vijana kuingia katika Sekta ya Kilimo na kuacha kuzunguka na bahasha ya kaki ya kuomba ajira sehemu mbalimbali nchini.
Hayo ameyasema Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga wakati mkutano wa waandishi wa habari kuhusiana na Kongamano la vijana  Kimataifa kuhusu Kilimo Biashara litakalofanyika Machi 20 hadi 22 katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa asilimia 60 ya wanafunzi wanahitimu vyuo vikuu wanakuwa sio wazalishaji  kutokana na kusubiri ajira hivyo Kilimo Biashara ndio suluhisho la ajira kwa vijana nchini.Hasunga amesema kuwa serikali imedhamiria kuweka mazingira ya Kilimo kwenda kisasa kwa kuhakikisha masoko ndani yanakuwa nafasi na ziada kuuza nje ya nchi.

"Vijana wakiingia katika Kilimo suala la kutembea na bahasha kwa ajili ya kutafuta ajira  litakuwa historia kwa kijana kuendesha Kilimo  hakihitaji watu wa kufanya usaili"amesema Hasunga.

Aidha amesema Kilimo kimekuewa kikilimwa kwa mazoea na kufanya kilimo kuonekana kigumu lakini serikali ya awamu ya tano tunakwenda na Kilimo cha kisasa kwa kuhusianisha masoko pamoja na viwanda kwa kwa ajili ya kuongeza thamani ya mazao.

Hata hivyo amesema kuwa vijana kwa kuwa na mwamko wa elimu huku wengine wakiwa wataalam watafanya chachu ya Kilimo na kufanya vijana  waliokata tamaa kuingia katika sekta ya Kilimo.Hasunga amesema nchi yeyote duniani inategemea vijana katika kupata Maendeleo  hivyo serikali haitaweza kuwaacha nyuma  katika sekta ya Kilimo.

Amesema takwimu zinaonyesha asilimia 53 ndio wanatumia jembe la mkono katika kilimo huku asilimia 27 wanatumia wanyama katika kuendesha takwimu na asilimia 20 wanatumia trekta .Nae Mwenyekiti wa Kongamano la Vijana Kimataifa Kuhusu Kilimo Biashara Majabi Emmanuel amesema kuwa  wanatarajia kuwa na washiriki 1000  kutoka sehemu mbambali wa ndani na nje ya nchi.

Amesema kuwa wameanda Kongamano hilo kutokana na vijana kujitenga katika kilimo wakati ndio chenye fursa ya kujiajiri moja kwa moja.
 Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akizungumza na waandishi habari kuhusiana na Kongamano la Kimataifa la Vijana   kuhusu Kilimo Biashara litafanyika Jijini Dar es Salaam.

Vijana wa Kilimo Biashara wakiwa na Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga mara ya kuzungumza na waandishi habari kuhusiana na Kongamano la Kilimo Biashara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...