Wafanyakazi wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), Moshi, wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya maazimisho ya siku ya wapendanao duniani ‘Valentine’s Day’ ambapo SBL imeazimisha siku hiyo kwa kuwakutanisha wanawake kujadili mchango wao katika ukuaji wa kampuni hiyo.
. Mwenyekiti wa wanawake wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Anitha Rwehumbiza akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya wapendandanao duniani (Valentine’s Day) ambapo SBL imeazimisha siku hiyo kwa kuwakutanisha wanawake kupitia jukwaa liitwalo ‘SBL spirited women’ ili kutambua mchango wao katika utendaji kazi wa kampuni hiyo.
Wafanyakazi wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), Moshi, wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya maazimisho ya siku ya wapendanao duniani ‘Valentine’s Day’ ambapo SBL imeazimisha siku hiyo kwa kuwakutanisha wanawake kujadili mchango wao katika ukuaji wa kampuni hiyo.

Katika kuadhimisha siku ya wapendano duniani maarufu kama ‘Valentine’s Day’ Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Ltd (SBL) imewakutanisha wafanyakazi wanawake wa kampuni hiyo ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wao katika utendaji kazi wa kampuni hiyo. 

Akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyofanyika leo Alhamisi Februari 14, 2019 Mwenyekiti wa wanawake wa SBL, Anitha Rwehumbiza amesema lengo kubwa ni kuwainua wanawake ndani na nje ya ofisi kupitia jukwaa maalumu lijulikanalo ‘SBL spirited women’. 

Hafla hiyo imefanyika katika makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Chang’ombe jijini hapa pamoja na matawi yaliyopo mikoa ya Mwanza na Moshi. 

“Lengo ni kuwainua wanawake katika nyanja tofauti sio tu katika kazi lakini pia nje ya ofisi na kwa mwaka huu tumeona tujumuike pamoja tuonyeshe upendo wetu kwa wanawake wote wa Serengeti na kuwashukuru wanawake kwa kazi kubwa waliyoifanya katika kuendeleza kiwanda chetu,” amesema Rwehumbiza. 

Rwehumbiza amesema katika siku hiyo ya wapendanao kampuni ya Serengeti inawakumbusha watanzania kuzingatia unywaji wa kiistaraabu. 

“Kwa wateja wetu tunawashukuru sana kwa kuwa pamoja na sisi kwasababu uwepo wetu unategemea zaidi wafanyakazi na vilevile wanywaji wetu wakubwa,” amesema 

Wanawake hao walionyesha umaridadi kwa kuvaa mavazi ya rangi nyekundu ambayo huvaliwa katika siku hiyo na kukabidhiwa kinywaji maalumu kijulikanacho kama ‘Baileys’ kinachotengenezwa na kampuni mama ya Diageo na kusambazwa na kampuni ya bia Serengeti. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...