MKUU
wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza wakati akizinduzi wa
kimkoa wa kampeni ya uwajibikaji katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi
mkoa wa Tanga ijulikanayo “jiongeze tuwavushe salama”
KATIBU Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi akizungumza katika uzinduzi hu
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Asha Mahita akizungumza wakati wa uzinduzi huo
MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akichangia jambo kwenye uzinduzi huo
MKUU wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa akizungumza wakati wa uzinduzi huo
MKUU wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe akizungumza jambo
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Asha Mahita kushoto akiwa na Mkuu wa
wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah mara baada ya uzinduzi huo ambao
uliwenda sambamba na uwekaji saini ahadi
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Asha Mahita kushoto akiwa na Mkuu wa
wilaya ya Korogwe Kisa Gwakisa mara baada ya uzinduzi huo ambao uliwenda
sambamba na uwekaji saini ahadi
MKUU
wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia akifuatilia utiaji wa saini na
kuweka ahadi Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Gissa Gwakisa akisaini
Wakuu
wa wilaya wakifuatilia kwa umakini uwasilishwaji wa taarifa mbalimbali
kwenye uzinduzi huo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu
Abdallah,Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa,Mkuu wa wilaya ya
Lushoto January Lugangika na Mkuu wa wilaya ya Kilindi Sauda Mtondoo
KATIBU
Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salim kulia akiwa na Katibu Tawala wa
wilaya ya Muheza Desderi Haule wakifuatilia kwa umakini uzinduzi huo
Katibu wa Afya Mkoani Tanga Abdiely Makange kulia akisisitiza jambo na mmoja wa washiriki wakati wa uzinduzi huo
Sehemu ya washirki wa uzinduzi huo wakimsikiliza kwa umakini mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella
SERIKALI
imeshauri kuchukuwa hatua za haraka ilikuweza kudhibiti tatizo la vifo
vya wajawazito nchini kuepuka kupoteza nguvu kazi kubwa ambayo ingeweza
kuwa msaada mkubwa kwa uchumi wa nchi.
Ushauri
huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela wakati Uzinduzi
wakampeni ya uwajibikaji katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi mkoa wa
Tanga ijulikanayo “jiongeze tuwavushe salama”
Alisema
kuwa takwimu za vifo vya wajawazito inaonyesha vinazidi kukuwa kila
siku hivyo wakati umefika sasa wa kuhakikisha serikali inashughuli kwa
haraka changamoto hizo ili kuweza kupunguza vifo hivyo.
“Kwa
mkoa wa Tanga pekee kwa kipindi cha mwezi mmoja tayari wajawazito nane
wamepoteza maisha hivyo kwa takwimu hizo inamaana mpaka mwisho wa mwaka
kutakuwa na vifo vingi “alisema RC Shigela.
Kwa
upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Zena Said alisema kuwa
miongoni mwa changamoto kubwa ni ukosefu wa miundombinu bora ya afya
kama vile gari la wagonjwa pamoja na uhaba wa wataalamu .
Vile
vile alisema kuwa changamoto nyingine mama mjamzito kutokwa na damu
nyingi,pamoja na kutopatiwa usaidizi wa haraka pindi pale anapokuwa
amefikishwa katika kituo cha afya kwa ajili ya huduma.
Hata
hivyo Mganga Mkuu wa mkoa Dkt Asha Mahita aliweza kutaja takwimu za
vifo kwa kipindi cha miaka minne ambapo kwa mwaka 2015 jumla ya vifo
vilikuwa 67.
“Kwa
mwaka 2016 kuliuwa na vifo 46 ,huku mwaka 2017 kukiripotiwa vifo
45,ambapo mwaka 2018 kukiwa na vifo 54”alibainisha Mganga Mkuu huyo.
Aidha
alisema kuwa mikakati iliyokuwepo ni kupeleka elimu kwa jamii kuona
umuhimu wa kuhudhuria cliniki kwa wakati,kushughulia kwa haraka
changamoto za vifo vitokanavyo na uzazi.
“Tumejipanga
katika kuhakikisha kila wilaya, huduma ya mama na mtoto inakuwa ni
kipaumbele chetu lakini pia kutenga bajeti kubwa ili kuweza kutatua kwa
haraka changamoto za wajawazito na watoto wachanga”alisema Dkt Mahita.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...